Hawa Ndio Wanasoka Wanaoongoza Kwa fedha nchini Kenya
Usajili wa kiungo wa kimtaifa wa Kenya ambaye pia ni nahodha wa timu ya
taifa Harambee Stars Victor Mugubi Wanyama kwenda klabu ya Southampton
toka klabu ya Glasgow Celtic umefanya orodha ya wachezaji wenye fedha
nyingi kuliko wote nchini Kenya kubadilika .
Nafasi ya tatu inashikiliwa na kaka mkubwa wa Victor Wanyama ambaye ni
McDonald Mariga . Mariga aliweka historia ya kuwa mchezaji wa Kwanza
toka Kenya na Afrika Mashariki kuvaa medali ya ubingwa wa Ligi ya
mabingwa na pia alikuwa mchezaji wa kwanza wa ukanda huu kucheza fainali
ya Ligi ya Mabingwa . Katika mishahara ya kawaida Mariga anashika
nafasi ya tatu lakini anaweza kuwa mchezaji mwenye utajiri kuliko wote
kwa kuwa amewekeza kwenye biashara nyingi nje ya soka ambazo zinamfanya
awe mchezaji tajiri kuliko wote kwenye ukanda huu. Kimshahara Mariga
analipwa milioni 77 za Kenya kwa Mwaka na hiyo inamfanya kuwa mchezaji
wa tatu anayelipwa hela nyingi .
Nafasi ya pili kwenye orodha hiyo inashikiliwa na nahodha wa zamani wa
timu ya taifa Dennis Oliech ambaye amecheza kwenye ligi ya Ufaransa
kabla kina Mariga na Wanyama hawajatoka nchini Kenya . Mshahara wa
Oliech kwa mwaka ni shilingi milioni 91 za Kenya ambazo kibongbongo ni
sawa na shilingi bilioni 1,693,305,779.42 9bilioni moja na milioni mia
sita tisini na tatu , laki tatu na mia saba sabini na tisa na senti
arobaini na mbili) . Kwa sasa Oliech anachezea Ac Ajaccio ya huko huko
Ufaransa .
Nafasi ya kwanza inashikiliwa na Wanyama ambaye kwa sasa pia ni mchezaji
ghali kuliko wote waliowahi kuuzwa wanaotoka nchini Scotland . Wanyama
analipwa mshahara unaokaribia milioni 250 za Kenya kwa mwaka kwa mujibu
wa mkataba wake ambao haujawekwa wazi kuonyesha atakuwa analipwa kiasi
gani kwa wiki.
No comments:
Post a Comment