Pages

Saturday, August 3, 2013

Usipitwe na mabadiliko haya ya Teknohama

 TEKNOHAMA SASA YAFIKIA KIWANGO HIKI

Maendeleo katika teknolojia ya mawasiliano hususani kwa vifaa vya matumizi ya mkononi kama vile simu yanazidi kuongezeka. Tunapoelekea ni kuwa watabaki watu wachache sana watakaotumia kompyuta za mezani (desktop computer), na hata laptop zinaelekea kupungua watumiaji, badala yake, watu wanaingia zaidi katika matumizi ya kompyuta ndogo na zinazohamishika toka sehemu moja kwenda nyingine. Katika makala yetu ya leo tunaangalia maendeleo makubwa tunayoyatarajia katika teknolojia ya mawasiliano:
Spidi kubwa ya mawasiliano:  Katika kurahisisha mawasiliano, wataalamu wamegundua teknolojia ya  LTE ( Long Term Evolution) ambayo pia huitwa 4G (4th Generation) ambayo ndio inayoelezwa kuwa tegemeo la kuifanya dunia iwe na mawasiliano ya kasi kubwa zaidi na kutokana na uwezo huo, basi vifaa vingi vitaweza kuunganishwa kupitia internet, na zaidi sana kuwezesha simu kufanya matumizi mengi ambayo yanafanyika sasa kupitia kompyuta kama vile kuangalia movie, kudownload movies hata za ukubwa wa 2GB, au hata kuangalia Youtube, n.k. Soma zaidi kuhusu teknolojia ya LTE katika makala yetu. 
 
Kuchaji simu bila kutumia waya:
Makampuni kadhaa kama vile ZTE, Google , AT & T, Starbucks na Nokia yamewekeza katika utafiti wa kuwa  na teknolojia itakayowezesha watumiaji wa simu kuchaji simu zao bila ya kuzichomeka ukutani . Kwa taarifa zilizopo kwenye mtandao wa Youtube, tayari Nokia wameshatoa simu zinazoweza kuchajiwa bila waya (wireless charging). Simu hizo za Nokia ni Nokia Lumia 920 na Nokia Lumia 820. Kampuni ya LG pia imetoa simu zake za LG Nexus 4 zinazotumia teknolojia ya wireless charging.
 
Website maalum za kuonekana kwenye simu:
Katika mabadiliko haya tunayoendana nayo ambapo watu wengi zaidi watatumia simu kuliko kompyuta, kuna haja basi ya kuwezesha websites ziwe na muonekano kama wa kwenye kompyuta za kawaida kwa watazamaji watakaotumia simu. Website hizo huitwa Mobile website. Kumbuka , kwa website kuwa Mobile website sio kwamba tuu eti inaweza kuonekana kwenye simu, hapana bali inakuwa imetengenezwa maalum kuwa na muonekano bora kwenye simu.
Mabadiliko yote haya yanamaanisha kuwa maisha yetu yanaenda kubadilika sana. Kuna ajira mpya na kuna watakaopoteza ajira au wateja. Mfano program mpya zinaendelea kubuniwa ili kurahisisha  matumizi ya simu ikiwa ni pamoja na kuwezesha simu kutype documents, kusave, kuprint, kama ambavyo watu wanafanya kwa kutumia desktop computer au laptops. Kwa wabunifu na watengenezaji wa website, wanatakiwa wajiboreshe katika kujua mabadiliko haya makubwa kwani tayari kuna muongozo wa jinsi ya kuprogram website ziendane na teknolojia za simu.
Wamiliki wa website na blogs wataanza kwa wingi kubadilika kuelekea kutumia teknolojia itakayofanya websites na blogs zao zionekane vema kupitia simu 

 
Mabadiliko yote haya yanamaanisha kuwa maisha yetu yanaenda kubadilika sana. Kuna ajira mpya na kuna watakaopoteza ajira au wateja. Mfano program mpya zinaendelea kubuniwa ili kurahisisha  matumizi ya simu ikiwa ni pamoja na kuwezesha simu kutype documents, kusave, kuprint, kama ambavyo watu wanafanya kwa kutumia desktop computer au laptops. Kwa wabunifu na watengenezaji wa website, wanatakiwa wajiboreshe katika kujua mabadiliko haya makubwa kwani tayari kuna muongozo wa jinsi ya kuprogram website ziendane na teknolojia za simu.
Wamiliki wa website na blogs wataanza kwa wingi kubadilika kuelekea kutumia teknolojia itakayofanya websites na blogs zao zionekane vema kupitia simu

Mwanamke mfupi kuliko wote duniani huyu hapa

Jina lake ni Jyoti Amge na anatokea India,ameingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness kama mwanamke mfupi kuliko wote duniani.

 image

Tetesi za kwenda kukipiga Santiago Bernabeu

USAJILI WA GARETH BALE UNAASHIRIA SIKU ZA CRISTIANO RONALDO KUBAKI SANTIAGO BERNABEU ZIPO SHAKANI


 Wakati Real Madrid wakiwa kwenye harakati za kuvunja rekodi ya usajili kwa kumsajili winga wa Tottenham Gareth Bale, uhamisho ambao unatoa ishara kwamba mwisho wa mchezaji waliyemlipia fedha nyingi zilizovunja rekodi ya dunia Cristiano Ronaldo unakaribia? Imekuwa ikiaminika kwamba Madrid wangeenda kumnunua Bale msimu huu ikiwa tu Ronaldo atataka kuondoka. Kwa sasa, mreno huyo anabaki kuwa mchezaji wa Real Madrid kwa asilimia mia, lakini kwa namna Madrid inavyoonesha kumhitaji Bale inaonekana siku za Ronaldo Bernabeu ni za kuhesabika.

Wakati tetesi za Ronaldo kurudi Manchester United ambazo zilitikisa sana mwanzoni mwa dirisha la usajili, sasa zinaonekana zimepoa, bado hatma yake ndani ya Madrid ipo shakani. Sababu kuu la hilo ni kwamba winga huyo mwenye miaka 28 anaingia kwenye miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake, hatua ambayo thamani ya mchezaji huanza kushuka, na ameonyesha hana nia ya kusaini mkataba mpya. Mara ya mwisho Ronaldo kuzungumzia mkataba wake na Madrid alisema kupitia mtandao wa Twitter kwamba 'taarifa zote za kusaini mkataba mpya ni za uongo'.

Huko nyuma, Ronaldo alizipa tetesi za kutaka kuondoka baada ya kusema kwamba hakuwa na furaha kwa sababu za kikazi ndani ya Madrid, kitu kilichotafsiriwa kwamba alikuwa akihitaji mashahara mkubwa na sapoti kubwa kutoka viongozi wa juu wa klabu. Mtu mmoja ambaye haamini kama suala hilo lilishaisha ni raisi wa zamani wa Madrid Ramon Calderon.

"Nafahamu kwamba hana furaha kabisa kwasababu ya tabia za Raisi," aliiambia Talksport Jumatano iliyopita. “Anataka mshahara wa €20 million kwa msimu jambo ambalo litakuwa gumu kwa Real kukubali.”

 
 
Na Calderon pia anaamini kwamba uhamisho wa kumleta Bale umechangiwa sana na sintofahamu ya hatma ya Ronaldo. “Nadhani raisi amejiandaa kwa kila kitu ikiwa atashindwa kumshawishi Ronaldo asaini dili jipya. Hivyo ndivyo ninavyoona. Anaogopa utafikia wakati Cristiano atasema 'sitaki kuendelea kuwa hapa'. Hiyo itakuwa habari mbaya kwa Madrid. Ningependa aendelee kuwa pale na kustaafu soka akiwa Bernabeu lakini kwa sasa hali ilivyo ni vigumu. Ngoja tuone wiki kadhaa zijazo mambo yatakavyokuwa.”

Maoni ya Calderon ambaye alihusika kwa kiasi kikubwa kumleta Ronaldo Madrid - na amekuwa akimtuhumu Perez kwamba kutokana hakuhusika katika kumleta mchezaji huyo ndio sababu ya kutompa sapoti mchezaji anayohitaji tofauti na ilivyo kwa wachezaji ambao alihusika na kuwanunua moja kwa moja, kitu ambacho kimewahi kumtokea hata Gonzalo Higuain.

Perez amekuwa akitaka kuonekana kwamba yupo nyuma ya Ronaldo kwa asilimia 100, na amekuwa akikaririwa akisema kwamba mchezaji huyo ataendelea kuwa Bernabeu na atamalizia mpira katika klabu hiyo - lakini nyuma ya kauli zake hizo ambazo zimekuwa zikitafsiriwa kuwa za kisiasa haswa hivi karibuni wakati ulipofanyika uchaguzi wa Madrid.

Wakati wakijiandaa kutoa fedha nyingi kuhakikisha wanamsajili Bale, inaonekana kama ni jambo la kamari kumfanya mchezaji ambaye ana uzoefu wa msimu mmoja wa champions league kuwa ndio star wa kikosi kinachotaka kubeba ubingwa wa ulaya kwa mara 10.

lakini pia uharaka wa kumleta Bale Bernabeu unatokana na hisia kwamba Ronaldo anaweza asiwe jijini Madrid kwa muda mrefu. Suala la Ronaldo kutokusaini mkataba mpya mpaka sasa haliwezi kuwa suala la Madrid kulichukulia poa. Kwa mchezaji hili suala ni faida kwake kwasababu mkataba unapokuwa unaelekea kuisha yeye anazidi kupata nguvu ya maamuzi dhidi ya hatma yake, wakati kwa upande wa Madrid wanajua wanapaswa kufanya wafanyalo kipindi hiki cha kiangazi walimalize suala la Ronaldo ikiwa wanataka kurudisha fedha zao walizolipa kumnunua la sivyo wanaweza kumuuza kwa kiasi kidogo au wakakosa kabisa ikiwa atabaki mpaka mkataba wake utakapoisha

Friday, August 2, 2013

Because following your dreams is all about you and your actions.

5 Reasons Why Your Dreams Don’t Come True

We all have dreams or things that we’ve always wanted to learn, but somehow never manage to accomplish them. Either it’s learning a foreign language, starting a blog about a hobby or improving some skills in a certain domain, there’s a lot out there each one of us has the desire to accomplish.
Some complain about not having the time to do it, while others follow their dreams. What’s their secret? What are their priorities? How do they manage with their time? Do they have more time available, or do they make time for things that are important to them?
Nobody really knows the answer. Because following your dreams is all about you and your actions. I won’t tell you what to do to accomplish your dreams. But I can tell you what’s stopping you from getting there:

 1. Bad time management

The main excuse that people find when they want to do something but don’t manage to is time. “I’m so busy that I don’t have the physical time to do it”, or “I don’t even have time for myself”. While that can be true in some cases, in most of them it’s just making excuses.
People rarely work at 100% capacity. I know persons that have all their day filled with activities and others which don’t do much of a thing besides the daily struggles for making a living. Neither case is healthy. It’s good to keep your day busy, but not until you reach exhaustion.

Also, being caught daily in the same routine certainly kills creativity or any desire for personal development. Try to find an equilibrium between the two. Of course everybody is tired after a busy day, but instead of sitting in front of the TV and watching some sitcom you might as well reserve that hour for something you always wanted to do.


2. Finding excuses

People feel frustrated when realizing time passes by and they’re filled with the regrets. That’s when excuses are being created. And honestly it’s perfectly normal: a panic reaction  when you try to find an explanation for your failure to accomplish something. Instead of trying to find excuses, focus on the future: try to figure out what factors are standing in the way of your dreams and actions. Because if you really want to accomplish something and you’re a perfectly healthy person capable of making his/her own decision, than nothing is standing in your way.

3. Procrastination

There’s always something more important to do, which requires your immediate attention. So you postpone your hobbies in favor of some extra hours of work, let’s say. Other times you postpone it because you’re not in the perfect mental/physical shape. You’re missing a lot in this way.
In this very inspirational article I was reading that education and intelligence accomplish nothing without action. It’s time to focus your energies also in turning your dreams into reality, not just preparing to do it.

4. Waiting for the right moment – when you’re prepared

One thing’s for sure: you’ll never feel more prepared for what you want. In fact, the longer you wait, the more insecure you’ll get and tend to postpone your actions. Instead of filling yourself with regrets and waiting for a moment that most probably won’t come, you could try instead making the first steps in a certain direction.

5. Not making your dream a goal – and forgetting about it

I want to do a lot of things. Some of them pass through my mind in most unusual moments. Unfortunately, , I quickly forget about them. But after a while I remember and in order not to forget again, I write them somewhere.
However, this doesn’t work: lists and lists all over again, and no checked marked to indicate that I’ve actually managed to bring any of them to an end. The reason for this is that people don’t always picture their desires as objectives. Instead of adding your desires to a list of “Things I want to accomplish, sometime, in the future”, you could try to visualize them as a clear objective.

Baada ya kumkosa Fabregas..

  MAN UNITED WAPO KWENYE MAZUNGUMZO YA KUMRUDISHA CRISTIANO RONALDO OLD TRAFORD

 
Real Madrid wapo tayari kumuuza Cristiano Ronaldo kwenda Manchester United mwezi huu baada ya nahodha huyo wa Ureno kukataa kuanza mazungumzo ya mkataba mpya.

Gazeti la Daily Star limesema United na Real Madrid wametumia siku 12 zilizopita kuzungumza juu ya ada ya uhamisho ya paundi millioni 80 - na mabingwa wa Premier League wamezidi kupata uhakika wa kumrudisha kipenzi chao Old Trafford. 

Raisi wa Real Florentino Perez mwanzoni alitaka kwamba uhakika kutoka kwa Ronaldo kama yupo tayari kusaini mkataba mpya - na alishangazwa kwamba mchezaji kuwa alikuwa tayari kurudi United. 

Hilo lilipelekea Madrid kufungua mazungumzo rasmi na United, wakitambua kwamba wanaweza wakamuuza kwa fedha kidogo ikiwa winga huyo atabakia kwamwaka mmoja zaidi ndani ya Bernabeu kwa kuwa atakuwa amebakisha mkataba wa mwaka mmoja tu.  

Lakini pia imeonekana wazi kwamba Madrid wanataka kumpata mbadala wa Ronaldo - Gareth Bale ambaye tayari wameshatoa ofa ya £85m kwa Spurs.
Mapema wiki hii aliyekuwa raisi wa Madrid - Ramon Calderon alikaririwa akisema kwamba Madrid wanajiandaa kumuuza Ronaldo na ndio maana wanafanya kila liwezekanalo kumsajili Gareth Bale kutoka Tottenham.

Ikumbukwe pia wakati akiwa bado kocha wa Man United Sir Alex Ferguson alikarriwa akisema kila kipo sawa kwa ajili ya usajili wa mchezaji mkubwa wakati wa dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa. Pia Wakati akihojiwa na BBC hivi karibuni aliyekuwa msaidizi wa Ferguson - Mike Phelan aliulizwa kama boss wake alikuwa akimzungumzia Ronaldo aliposema kuhusu usajili wa mchezaji mkubwa? Phelan alishindwa kukataa wala kukubali kuhusu suala hilo, akisema "no comment'.

Mcheki Dogo Huyu...

MCHEKI MTOTO "SAMBATH UON" MWENYE MIAKA SITA ANAVYOCHEZEA CHATU 

 Sambath Uon ni mtoto mwenye miaka sita (6)  amefanya mambo ya kushangaza dunia anaishi katika kijiji cha Cambodia, Asia ya kusini pia nyoka huyu ana urefu wa mita 8m (26 ft) na uzito 180 kg (400 lb)