CRISTIANO RONALDO ASAFIRI MPAKA GALICIA KWENDA KUCHANGIA DAMU KWA MAJERUHI WA AJALI YA TENI
Kwa mujibu wa ripoti katika vyombo vya habari za Spain - Cristiano Ronaldo alisafiri kutoka jijini Madrid kwenda mpaka ilipotokea ajali ya treni huko Galicia na kwenda kuchangia damu kwa majeruhi wa ajali ya hiyo ya treni iliyotokea karibu na kaskazini mashariki mwa Santiago de Compostela.
Inasemekana kulikuwepo na majeruhi zaidi ya 160 huku watu wengine 0 wakifariki dunia.
Pamoja na kuripotiwa kufanya kitendo hicho, nyota huyo wa Real Madrid alitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kutoa pole kwa wahanga wa ajali hiyo
Aliandika
“Ninaungana na ndugu jamaa na marafiki wa wahanga wa ajali na nawaomba watu wengine mkasaidie majeruhi wa ajali hiyo. #animogalicia”
No comments:
Post a Comment