Paris Jackson ajaribu kujiua
Bintiye marehemu Michael Jackson, Paris, mwenye unmri wa miaka 15,
amelazwa katika hospitali moja mjini Carlifornia baada ya kujaribu
kujiua. Msemaji wa familia ameeleza kuwa anaendelea kupata nafuu na kuwa
madaktari wanamshughulikia vilivyo.
Inasemekana, Paris Jackson, ambaye babake alifariki mwaka 2009, amekuwa katika hali ya kusononeka kwa muda sasa.
Msemaji alifafanua kuwa hali yake si mbaya sana ya kupelekwa kwa wadi ya wagonjwa mahututi. Msemaji wa familia hiyo amesema kuwa usiku wa kuamkia leo binti huyo alikimbizwa hospitalini baada ya kujaribu kujiua lakini anaendelea kupata nafuu.
Paris Jackson ametajwa kama mmoja wa familia ya Michael Jackson
anayetaka kulipwa mamilioni ya Dollar kutoka kampuni ya AEG ambayo
ilimwajiri daktari aliyempa madawa Michael ambayo yaligunduliwa baadaye
kuwa yalimwua.
Kesi inayohusiana na madai hayo imeendelea kwa majuma sita sasa. Mengi
ya kusikitisha juu ya Michael Jackson yamekuwa yakitajwa na inadhaniwa
kwamba yamechangia pakubwa kupandisha huzuni na simanzi kwa msichana
Paris.
Inadhaniwa kuwa Paris amejaribu kadiri ya uwezo wake kumwomboleza baba
yake lakini angali anasononeka kutokuwepo kwake. Mlezi wake kisheria ni
nyanya yake Catherine lakini hata hivyo siku chache zilizopita amekuwa
akiishi na mama yake mzazi.
No comments:
Post a Comment