WANAKIJIJI WA CHAMWINO WALIA NA NJAA
VIJIJI vyote
77 vya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma
vimekumbwa na baa la njaa kutokana na ukame mkali uliodumu kwa miezi
miwili mfululizo.
Ukame huo ulio ulioanza mwanzoni mwa mwezi wa kwanza
mpaka mwishoni mwa mwezi wa pili
umefanya hali ya chakula kuwa mbaya Wilayani humo hali inayozidi kutishia
maisha ya watu.
Akitoa taarifa ya hali ya chakula Afisa kilimo wa
Wilaya ya Chamwino kwenye Baraza la Madiwani lililofanyika jana Gofrey Mnyamale alisema kutonyesha Mvua kwa kipindi hicho
kumesababisha hata zao la Mtama ambalo
huwa linastahimili ukame kukauka.
Alisema katika msimu wa kilimo wa Mwaka 2012/13 wilaya
ilijiwekea malengo ya kulima Hekta 118, 071 za mazao ya chakula na kutarajia
kuvuna tani 105, 040 kama Mtama, Mahindi
na uwele lakini malengo hayo yamepotea.
Aliongeza kuwa Mvua nyingi zililizonyesha katika
mtiririko usioridhisha hasa Mwezi Desemba na kufuatia na ukame mkali katika
miezi hiyo miwili kuliwapoteza watu waliozoea kupanda mapema kutokana na hali
ya hewa ya mkoa wenyewe.
Mnyamale alitanabaisha kuwa waliamua kuwaagiza
wananchi kutunza chakula kidogo walichonacho, wenye mifugo kuuza ili kununua
chakula, kuzuia wafanyabiashara wasitoe nje chakula na kufanya tasmini ya kina
ili taarifa ipelekwe kwa Waziri mkuu mapema iwezekanavyo.
‘’Tunataka baada ya kukamilisha Tathimini hii Taarifa
itapelekwa haraka kwa Waziri Mkuu ili hatua za haraka za kunusuru watu dhidi ya
janga la njaa zichukuliwe mapema mapema
iwezekanavyo ambapo tunatarajia kabla Mei
10 mwaka huu kuwa imekamilika’’, alisema
Kwa upande wake Mjumbe wa NEC ya CCM Samwel Malecela
aliitaka Serikali kuchukua hatua za Haraka ili kunusuru hali ya njaa katika
Wilaya nyingi kutokana na upungufu wa chakula kuwa kila sehemu.
‘’ Janga hili ni kubwa na Mara nyingi Serekali imekuwa ikisema
inafanya upembuzi yakinifu na inatumia muda mwingi kupembua katika hili
nawaambia wafanye haraka kwani hali ni mbaya mno bora kitu kingine kuliko njaa’’,
alisema
Malecela Aliongeza kuwa yeye kwa nafasi yake
anatembea kila wilaya na amebakiza chache ili amalize na sehemu kubwa inatatizo
la kukosa chakula hivyo serekali ihakikishe inatoa kipaumbele kuanzia na wilaya
zilizoathirika sana kama hiyo ya Chamwino anakotokea.
No comments:
Post a Comment