Tunayemtaka ni Wayne Rooney tuu..!! - Mourinho
Kocha wa Chelsea Jose Morinho amethibitisha dhamira ya kumsajili
mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney
baada ya kutoa kauli kuwa
”
Tunayemtaka ni Wayne Rooney pekee”.
Kauli hii inakuja huku zikiwa
zimepita saa chache baada ya Manchester United
kuikataa ofa ya Chelsea
ya Paundi milioni 10 kwa ajli ya mchezaji huyo .
Jose Mourinho akiteta jambo na mkurugenzi wa Chelsea Ron Gourlay huko Bangkok , Thailand .
Hata hivyo Chelsea imezikanusha taarifa kuwa Ilikuwa Tayari kuwatoa
mmojawapo kati ya David Luiz na Juan Matta kama sehemu ya dili la
kumnunua Rooney. Mustakabali wa Rooney unaonekana kuwa story ya “Msimu
huu wa usajili” baada ya kuwepo na kauli tata juu ya maisha ya mchezaji
huyo ndani ya klabu ya ya Manchester United .
Pamoja na haya , bado mabingwa hawa wa England (United) wameendelea kushikilia msimamo wao kuwa mchezaji huyo hauzwi .
No comments:
Post a Comment