Pages

Tuesday, July 16, 2013

Kutoka Kenya

Wakulima wa Miraa Kenya wahofia marufuku 

 

Uamuzi wa serikali ya Uingereza kupiga marufuku Miraa (Khat) baadae mwaka huu unakabiliwa na upinzani mkali nchini Kenya kutoka kwa wakulima wa mmea huo unaosemekana kulewesha ingawa kwa kiwango kidogo sana. Huku jua likichimoza mjini Meru, maeneo ya mlima Kenya , wakulima wa Miraa ndipo nao wanaanza kazi.
Wanaume kumi na wawili hivi, baadhi wakionekana kula chuvi nyingi, wanapanda miti kwa uangalifu mkubwa, hii ni biashara inayohitaji uangalifu mkubwa.
Wanataka majani yanayoonekana kuwa machanga kwa hivyo itawabidi kupanda hadi juu kabisa ya mti na lazima waharakishe.
"kazi hii huwa twaifanya asubuhi na mapema , inahitaji kupelekwa sokoni nbaada tu ya kuyachuna,'' anasema Jeff Kubai.
Katika kazi yake ya mchana bwana Kubai ni prefoesa wa saikolojia.
Lakini kama wengi hapa, yeye hupanda Miraa au Khat kama yanavyojulikana hapa.
Familia yake imekuwa ikipanda Miraa kwa miaka mingi. "ni mmea, ambao unalewesha kidogo na kumfanya mtu kuwa na furaha isiyo na kifani,'' anasema huku akitafuna majani hayo. Miraa lazima ipate kuuzwa haraka wakati majani yake yakiwa hai.


 
Lakini katika eneo hili, utafunaji wa Miraa ni jambo ambalo lina mizizi yake katika tamaduni za Meru.
"Mashujaa zamani walikuwa wakitafuna Miraa," asema bwana Kubai, "ili kuwaogopesha maadui na pia kuwalinda mifugo malishoni.''
"Viongozi wa jamii zamani pia walikuwa wakitafuna Miraa wakati wakijadili mambo yanayohusu jamii.''
Tunahisi uchungu sana na kama tumesalitiwa. Tunamtaka waziri wa mambo ya ndani Uingereza kubatili uamuzi wake, aliongeza Kubai''
Utafunaji Miraa umeenea kote Meru, huku asilimia 80 ya wenyeji wakiwa wanategemea sana biashara ya Miraa kama pato lao la maisha.
"Hili shamba hunipatia mazao ya thamani ya dola elfu mbili miatatu ,'' anasema Kubai
"Hizi ndizo pesa nilizotumia kujenga kanisa, kusaidia watoto mayatima na miundo mbinu mingine na mambo mengine muhimu.
"Yaani kwa kifupi tu miasha ya watu hapa yanategemea miti hii.''
Na ndio maana viongozi wengi wa hapa wamepinga vikali hatua ya Uingereza kupiga marufuku biashara ya Miraa na kusema ni dawa ya kulevya iliyo kwenye kiwango cha C
Omar Ahmed ni mfanyabiashara wa Miraa kutoka jamii ya wasomali ambao hutumia sana Miraa.
Kiwango kikubwa cha Miraa inayouzwa Uingereza takriban asilimia 15 hutoka Meru na ina thamani ya dola milioni 7.5.
Bwana Ahmed anakabiliwa na hasara kubwa.
"Tutafanya kila tuwezalo, kuonyesha serikali ya Uingereza kwamba ikiwa hawatajali maslahi yetu wasitarajie kuwa na sisi tutajali maslahi yao, anasema Ahmed huku akitafuna majani hayo.
Kila mtu hapa aneonekana kutafuna Miraa kwa masaa kadhaa , na sasa hasira inapanda.

Bwana Ahmed mwenyewe anaonekana amelewa kidogo.
Lakini kuna mengi zaidi kuhusu swala hili kuliko vitisho vya mfanyabiashara huyu.
Mbunge wa eneo hili Kubai Kiringo, anasema kuwa Kenya huenda ikatafakari upya 

kuhusu uhusiano wake na Uingereza ikiwa haitabatilisha, uamuzi wake.
Miraa baada ya kutolewa shambani huwekwa ndani ya magunia meupe na kusafirishwa hadi Nairobi na kwingineko.
Wakati marufuku hiyo itakapoanza kutekelezwa baadaye mwaka huu, sera ya Uingereza itakuwa sawa na ile ya Marekani, Canada na nchi nyinginezo za Muungano wa Ulaya zote ambazo zimeitaja Miraa kuwa dawa ya kulevya.

No comments:

Post a Comment