LIVERPOOL YAMUWEKEA NGUMU LUIS SUAREZ BILA PAUNI MILIONI 40 HAONDOKI
LIVERPOOL haitakubali ofa yoyote chini ya pauni milioni 40 kwa ajili ya
kumuuza mshambuliaji wake raia wa Uruguay, Luis Suarez anayetaka
kuondoka Anfield.
Jumatano iliyopita iliripotiwa kuwa miamba ya Hispania, Real Madrid
inajipanga kupeleka ofa ya pauni milioni 40 baada ya ofa ya Arsenal ya
pauni milioni 30 kutolewa nje.
Arsenal ambayo imeamua kumfanya Suarez lengo lake kuu la usajili baada
ya kuonekana kukwama kumtwaa mshambuliaji wa Madrid, Gonzalo Higuain
ambaye kocha wake mpya Carlo Ancelotti anataka kumbakisha, inaelezwa
kujipanga kupeleka ofa nyingine ya pauni milioni 35.
Lakini bado Arsene Wenger anakabiliwa na kizingiti kwa kuwa Liverpool
haitakubali ofa ya chini ya pauni milioni 40, na kwa kuwa mkataba wa
Suarez unakwenda hadi mwaka 2016, klabu hiyo haina presha ya kumuuza –
licha ya matakwa yake.
Suarez, 26, atakosa mechi sita za kwanza za msimu mpya wa Premier League
wakati akimaliza adhabu ya kukosa mechi kumi msimu uliopita baada ya
kumng’ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic na anatarajiwa kujiunga na
kikosi chake wiki ijayo
No comments:
Post a Comment