Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa lajadili Usalama wa Waandishi wa Habari
Bwana Mustafa Haji Abdinur
mwandishi kutoka Somalia anayeandikia AFP akizungumza mbele ya Baraza
Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, wakati Baraza hilo siku ya Jumatano
lilipojadili usalama wa waandishi wa habari katika maeneo yenye
migogoro, Bw. Abdinur ambaye amejifundisha mwenyewe uandishi wa
habari alieleza kwamba pale alipo ni kama maiti inayotembea na kwamba ni
suala la muda tu yeye kuuawa kutokana na ukweli kwamba waandishi
wenzake wengi wamekwisha kuuawa nchini Somalia. Hii ili kuwa ni mara ya
kwanza kwa waandishi wa kimataifa kuzungumza ndani ya Baraza hilo.
-
Baraza Kuu la Usalama la
Umoja wa Mataifa, jana jumatano liliendesha majadiliano ya wazi kuhusu
usalama wa waandishi wa habari katika maeneo yenye migogoro.
Majadiliano
hayo yaliratibiwa na Marekani ambaye ni Rais wa Baraza hilo kwa mwezi
huu wa Julai, na kuhudhuriwa na waandishi wanne wa kimataifa ambao
walipata fursa ya kuelezea masahibu wanayokumbana nayo wakati wa
kitekeleza majukumu yao.
Majadiliano kuhusu suala la usalama wa
waandishi wa habari katika maeneo yenye migogoro ni ya kwanza kufanyika
ndani ya Baraza hilo, tangu lilipopitisha Azimio namba 1738 mwaka 2006
lililokuwa likizungumzia suala hilo. Aidha hii pia ni mara ya kwanza
kwa waandishi wa kimataifa kuzungumza ndani ya Baraza Kuu la Usalama.
“Hapa
nilipo mimi ni maiti anayetembea, ninatembea pasi kujua nani anaweza
kuondoa uhai wangu,wakati wowote naweza kupotea maisha. naweza kuuawa
hata na kijana mdogo ilimradi ana silaha”
Kauli hiyo ilikuwa ni
ya Bw. Mustafa Haji Abdinur anayeandikisha AFP akitoka Somalia. Na
kuongeza kwamba rafiki zake wengi ambao ni waandishi wenziye tayari
wameshapotea maisha na kwamba kwa yeye kuwa hai mpaka sasa ni kama bahati lakini ni suala la wakati tu.
Bwana Richard Engel kutoka NBC
News mmoja kati ya waandishi wanne walioalikwa na Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa kueelezea uzoefu wao na mikimikiki wanayokumbana nayo
wanapotekeza majukumu yao ya kiuandishi. Bw. Engel ambaye amesema
amewahi kutekwa, alilitaka Baraza Kuu la Usalama linapojadilia kuhusu
dhana nzima ya usalama wa waandishi, kujadili pia ni nani hasa
mwandishi wa habari anaye stahili ulinzi na akahoji kama wanaharakati
ambao nao wanachukua picha za matukio mbalimbali na kuzipost kwenye
mablog kama nao ni waandishi wa habari. pembeni yake ni Bi. Kathleen
Carroll, ambaye ni mhariri mtendaji wa Associated Press na Makamu
mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya Kulinda Waandishi ( CPJ) yeye katika
mchango wake alisema licha ya kwamba waandishi wengi wanapoteza maisha
wakati wakitafuta habari kwenye maeneo yenye migogoro lakini waandishi
watano kati ya sita wanauawa ndani ya nchi zao wakati wakitimiza
majukumu yao.
--
Naye
Bi. Cathleen Carrol ambaye ni Mhariri Mtendaji wa Associated Press
na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya Kuwalinda Waandishi ( CPJ)
pamoja na kuelezea kwa uchungu mkubwa matukio ya mauaji
yaliyowakumbua waandishi wenzake katika maeneo mbalimbali duniani
anasema, katika shirika lao kuna eneo ambalo limetengwa maalum
kwaajili ya kuwaenzi waandishi wote ambao wamepoteza maisha katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Kwa
upande wake, mwandishi Richard Engel wa NBC news, yeyé pamoja na
kuelezea mikasa mbalimbali ambayo amekwisha kumbana nayo yakiwamo ya
kutekwa wakati akiripoti matukio ya migogoro, yeyé alikwenda mbalia
zaidi kwa kuuliza ni nani hasa mwandishi wa habari.
Bw,
Engel alieza kwamba ulinzi wa waandishi wa habari hivi sasa unakuwa
mgumu sana tofauti na miaka ya nyuma kutokana na kile alichosema
kuibuka kwa makundi mengi yanayofanya kazi za waadishi wa habari.
“
Wakati tukijadili hoja hii ya usalama wa waandishi wa habari, pengine
pia ni muhimu tukajiuliza hivi ni nani hasa mwandishi wa habari, je
mwanaharakati anaye shika video au kamera na kalamu je naye ni
mwandishi, au je na yule mwanamgambo mwenye silaha lakini naye
ameshika kamera na kupiga picha je naye ni mwandishi” akahoji Bw,
Engel
Anasema kwamba
ni jambo la kawaida hivi unapokwenda kwenye tukio fulani kukutana na
makundi ya watu kila mmoja akiwa ameshika kamera yake akichukua matukio,
na katika mazingira kama haya, ni vigumu kwa vyombo vya ulinzi na
usalama kutofautisha nani hasa ni mwadishi aliyesomea na kubobea kwenye
fani hiyo na yupi mwanarakati.
Kwa
maoni yake anasema pamoja na hamu ya kila mtu kutaka kutaka
kukukusanya habari na kuzisambaza kupitia mitandao ya kijamii, ni vime
kujiuliza nani anastahili na anapwashwa kupewa ulinzi anapotimiza
majukumu yake na kwa vyovyote vile anasema kama ilivyo kwa
wanadiplomasia ambao wanakinga vilevile waandishi waliosomea na wenye
weledi na taaluma yao wanatakiwa kupewa ulinzi.
Majadiliano
hayo yalifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan
Eliasson, na yalikuwa na mvuto wa ina yake hasa kutoka na kauli
zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya wachangiaji.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu alieleza kwamba hujuma dhidi ya
waandishi wa habari ni jambo lisilokubalika kwa kile alichosema ni
kubinya uhuru wa upatikanaji na utoaji wa habari, lakini pia ni
ukiukwaji wa uhuru wa kujieleza. Akalipongeza Baraza kwa kuitisha
mjadala huo
Akasema
karne iliyopita waandishi wa habari wapatao 600 walipoteza maisha
katika matukio mbalimbali na wengine wakiishia magerezani, huku
asilimia 90 ya matukio hayo hakuna hatua zozote za kisheria
zilizochukuliwa.
Pamoja
na wachangiaji wengi kukiri kwamba mazingira ya ufanyaji kazi kwa
waandishi wa habari yamezidi kuwa magumu na hatari, walielezea pia
kwamba mazingira hatarishi hayapo tu katika maeneo yenye vita bali
hata katika nchi wazofanyia kazi. Ambapo takwimu kutoka CPJ
zinaonyesha katika kila waandishi watano kati ya sita wanauliwa wakiwa
ndani ya nchi zao.
Wengi
wa wazungumzaji walieleza kwamba baadhi ya waandishi ama wamekuwa
wakitishiwa maisha yao na familia zao au hata kupoteza maisha kwa
kuandika na kuchapicha habari zinazofichua vitendo vya rushwa ,
vitendo vya jinai au kashfa zinazohusu makundi mbalimbali ya jamii na
vilevile kuandika habari za uchochezi kati ya kundi moja na jingine..
Wengine
wakaenda mbali kwa kusema wakati mwingine waandishi wenyewe wanajiweka
katika mazingira ya hatari kwa kukiuka misingi ya kazi zao, kwa
kuandika habari zinazopendelea upande mmoja, au kufanya kazi kinyume
cha matakwa na matarajio ya yule anayemfanyia kazi.
Wazungumzaji
hao wakatoa wito kwa Baraza kuu la Usalama kuangalia namna bora ya
kuboresha ulinzi wa waandishi wa habari katika mazingira hatarishi kama
vile vita na migogoro na pia wakatoa wito wito kwa waandishi wa habari
kuzingatia misingi ya taaluma zao na kuepuka kujingiza katika mitengo
isiyo ya lazima.
Suala
lingine lililozungumwa kwa kina ni lile la kutofikishwa mbele ya mkono
wa sheria watu wanaotuhumiwa kuwahujumu waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment