Pages

Wednesday, July 31, 2013

Usome ujumbe huu alaf kisha nahitaji maoni toka kwako

Siku moja punda wa mkulima alianguka ndani ya kisima. Mnyama huyo alipiga kelele kinyonge kwa masaa kadhaa wakati mkulima akijaribu kufikiri nini cha kufanya.
 
Hatimaye, aliamua kwakuwa punda wake alikuwa mzee, na pia kisima hicho kilihitaji kufunikwa juu, Akaona hapakuwa na haja ya kumtoa.
 
 
Akaita majirani zake wote waje kumsaidia. Wao wote wakachukua makoleo na kuanza kuchota taka kwa koleo na kuzitupia ndani ya kisima.
 
Mara ya kwanza, punda aligundua nini kilikuwa kinatokea akapiga kelele kwa nguvu. Basi, ikawashanganza wale watu punda aliponyamaza ghafla!
Baada ya kutupa taka kadhaa kwenye hicho kisima. Huyo mkulima alishangazwa na kile alichokiona. Kwamba kila koleo la taka lililorushwa juu ya mgongo wa punda, punda alikuwa akifanya kitu cha kushangaza. Alikuwa akijitikisa ili taka zimwagike chini huku akipiga hatua moja kutoka shimoni.

Kadri mkulima na majirani walivyoendelea kutupa uchafu kwa koleo juu ya punda yule, alizidi kutikisa mgongo wake na kupiga hatua moja kuja juu. Muda mfupi baadae, kila mtu alishangaa jinsi punda alivyozidi kutokeza ndani ya kisima na kuja juu.



FUNZO:
Maisha yatakutupia kila aina ya uchafu. Ili utoke nje ya kisima wahitaji kujitikisa na kuchukua hatua moja juu. Kila tatizo ulilonalo, ni jiwe la kukuwezesha kukanyaga na kupiga hatua kuja juu. Tunaweza kutoka nje ya kisima kirefu kwa kuongeza bidii ya kupiga hatua moja kuja juu bila kuacha na kutokata tamaa kamwe. Tikisa uchafu mbali na kuchukua hatua kuja juu.

 
Kumbuka kanuni 5 rahisi ili uwe na furaha:

 
1. Weka huru moyo wako mbali na chuki - Samehe.

2. Weka huru akili yako mbali na wasiwasi - Wengi hushindwa kabisa kipengele hiki.

3.Tosheka / ridhika na ulichonacho.

4. Toa zaidi.

5. Tarajia vichache kutoka kwa watu lakini zaidi kutoka kwako mwenyewe.

No comments:

Post a Comment