Pages

Sunday, July 28, 2013

Nitaikataa ofa mpya ya UNITED kumnunua FABREGAS


KOCHA MPYA WA BARCELONA AIKATAA OFA YA UNITED KUMNUNUA FABREGAS

 
Gerardo Martino amemwambia David Moyes kwamba Cesc Fabregas hauzwi baada ya kutambulishwa rasmi kuwa kocha mpya wa klabu ya FC Barcelona kwa mkataba wa miaka miwili.

Kocha huyo wa zamani wa Newell's Old Boys amerithi mikoba ya Tito Vilanova, ambaye alilazimika kujiuzulu kutokana matatizo yake ya kiafya.

Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari Ijumaa, Martino alisema: 'Man United inamtaka Cesc? Kama klabu ilikataa ofa mbili za kwanza, mie nitaikataa ya tatu. Cesc atabaki hapa.'

Makamu wa Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu amethibitisha maneno ya Martino, akiongeza: 'Ni kawaida United kuvutiwa na mchezaji, lakini tunamtegemea Cesc na hatutomuuza, haijalishi watatoa ofa ya kiasi gani.

No comments:

Post a Comment