Pokea Haya Maujanja 15
1. Wafungwa walioko kwenye gereza la watu wenye makosa ya
ugaidi huko Guantanamo bay cuba hupewa misosi ya nguvu toka kwenye
migahawa ya McDonalds pale wanapoonyesha ushirikiano wa kufichua siri
wakati wakihojiwa.
2.Unaweza kutibu maumivu ya kichwa kwa kusugua kipisi cha limao kwenye paji la uso.
3. Inasemekana kuwa asilimia 60 ya wanawake walioko ndani ya
ndoa afya yao kimwili na kiakili sio nzuri kutokana na matatizo
yanayohusiana na ndoa.
4.Hii inawahusu wale watu ambao wanapenda sana kuchat kwenye
simu zao mpaka kufikia kusikia milio ya simu au vibration vichwani mwao
hata pale ambapo hakuna msg au simu iliyopigwa, watu hawa wanaugua
ugonjwa wa kisaikolojia unaitwa TEXTAPHRENIA.
5. Producer Dr. Dre hakuwahi kufahamu au kugundua kama Eminem ni mzungu mpaka siku waliyokutana.
6. Wanawake ambao hukumbwa na msongo wa mawazo wakati wa uja uzito wao wana hatihati ya kuzaa watoto wenye hasira kali.
7. Unaambiwa kwa kila hatua moja ambayo unatembea unatumia misuli 200 ambayo yote kwa pamoja hukusaidia kuitengeneza hiyo hatua.
8. Wakati Mohamed Ali anaanza kuingia kwenye mchezo wa ngumi,
Mwalimu wake ambaye alikuwa mzungu alimkatisha tamaa akimwambia kuwa
hawezi kufanikiwa kwenye mchezo huo… hiki kitendo kilimpa hasira bondia
huyu na alipofanikiwa kushinda medali yake ya kwanza ya OLYMPIC
alimzawadia mwalimu huyu na kumkumbusha maneno yake, hii ni fundisho kwa
kila mmoja kwamba usikubali mtu akukatishe tamaa kwenye ndoto yako.
9. Marapa wawili toka New York Busta Rhymez na Jay Z
waliowahi pia kuja Tanzania kufanya matamasha kwa hisani ya Clouds Fm na
Prime time promotions, waliwahi kusoma shule moja ya sekondari na siku
moja walishindansishwa kwenye zile rap freestyles kwenye Mgahawa wa
shule hiyo na Jay Z aliibuka mshindi, kitambo sana ilikuwa… rapa
mwingine ambae ni Christopher Wallace au Notorious BIG naye alikuwa
mwanafunzi kwenye hiyo shule.
10. Hii ni kwa watu wangu wanaovuta fegi au sigara, Unaambiwa
kila sigara moja unayovuta inapunguza urefu wa maisha yako kwa angalau
dakika kumi na moja .
11. Mitandao ya ngono imekuwa moja ya biashara zinazoongoza
kwa kuingiza fedha kutumia Internet ambapo katika kila sekunde kuna dola
elfu tatu na sabini na tano za kimarekani hutumiwa kwenye mitandao
hiyo.
12. Unaambiwa Jina maarufu la kiume kuliko majina yote
ulimwenguni ni Mohamed, inakadiriwa kuwa kuna Wanaume zaidi ya milioni
150 duniani waliopewa hili jina.. Muhammad was the most common
baby boy name in England and Wales in 2009, 2011 and 2012 and the second
most popular in 2007 and 2010, combining 14 spelling variations
13. Mvumbuzi wa balbu au taa Tomas Edison Alva alikuwa muoga
sana wa giza na ndio maana akafanya juu chini mpaka akatengeneza taa.
14. Mwanadamu huzaliwa na mifupa 300 mwilini mwake lakini
mpaka anafikia hatua ya utu uzima hubakiwa na mifupa 206 pekee,
unaambiwa hiyo mingine inapungua kutokana na kuunganika kadri umri
unavyosogea.
15. Enzi za kale nchini Uingereza kulikuwa na sheria
inayoitwa sheria ya dole gumba au The rule of the thumb ambayo ilikuwa
inaamuru kuwa mwanaume au mume kutoruhusiwa kumpiga mkewe na kitu
kikubwa zaidi ya kidole gumba.
No comments:
Post a Comment