Mmarekani wa kwanza kuwahi kumiliki Mabilioni ya Dola
John Davison Rockefeller aliwahi kushikilia
rekodi ya kuwa Mwanaume tajiri duniani lakini pia Muamerika wa kwanza
kuwahi kumiliki mabilioni ya dola ambapo mwaka 2007 mtandao wa Forbes
ulirekebisha utajiri wa John Rockefeller baada ya mfumuko wa bei na
kukadiria kwamba alikuwa na utajiri wa dolla billion 663.4
Unaambiwa In 1870, he founded Standard Oil Company and aggressively ran it until he officially retired in 1897
John Rockefeller alifariki mwaka 1937 May
23 huko Florida akiwa na miaka 97, utajiri wake umetokana sana na
biashara ya mafuta ambayo kwa kipindi hicho ndiyo ilikuwa nishati mpya
na inahitajika sana, alianzisha kampuni inaitwa Standard Oil Company
ambayo iliweza kufanikiwa kutawala soko la mafuta kwa kiasi kikubwa
sana, baada ya biashara kwenda vizuri akiwa na ndugu zake wa karibu…
John Rockefeller aliweza kuwa Mmarekani wa kwanza kufikisha utajiri wa
dola billioni moja.
Zaidi ya biashara, John Rockerfeller
alitumia utajiri wake mwingi kwenye ku-invest ndani ya masuala ya
utafiti wa kisayansi kwenye mambo ya dawa za binadamu, elimu na kusaidia
watu kwenye foundation yake ambapo kwenye research alizowahi kuwekeza
pesa zake na kuweza kupata mafanikio makubwa hasa kwenye kutokomeza
janga la homa ya manjano kipindi hicho na minyoo inayoitwa hookworm.
Kumbukumbu ya John Rockefeller kwenye sekta
ya elimu bado ipo hadi leo kwasababu ndiye mwazilishi wa vyuo vikuu
Marekani kama University of Chicago na Rockerfeller University.
No comments:
Post a Comment