Pages

Friday, July 12, 2013

Balotelli


BALOTELLI ATISHIA KUNUNUA KIFARU KWA AJILI YA WASUMBUFU BARABARANI

 
Mshambuliaji wa AC Milan, Mario Balotelli ametishia kununua kifaru kwa ajili ya kuwakomesha wasumbufu barabarani.

Balotelli ambaye ni tegemeo katika kikosi cha timu ya Italia, ameweka maneno hayo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.
Muitaliano huyo anayefuatiliwa na watu wapatao milioni moja ameamua kutoa kichekesho hicho ikiwa ni sehemu ya kitisho kwa watu ambao hata hivyo hakuwataja.

Aliweka maandishi haya, 'When some one is driving a Ferrari and he flash you than, just get the f*** out of the way! Pff (in case I would do the same). 'Or maybe I should just buy a TANK!'
Halafu akaweka picha ya kifaru ambacho kinapita juu ya gari, kuonyesha atafanya hivyo kwa ambao watakuwa wasumbufu barabarani.
Balotelli amekuwa maarufu kutokana na vituko lukuki hasa katika kipindi alichokuwa anachezea Manchester City ya England kabla ya kuamua kuondoka na kurejea kwao Italia.

No comments:

Post a Comment