RAIS WA BAYERN MUNICH ASHITAKIWA KUKWEPA KODI
Wiki kadhaa baada ya mchezaji bora wa dunia Lionel Messi kutuhumiwa kukwepa kulipa kodi, sasa raisi wa mabingwa wa ulaya Bayern Munich Uli Hoeness ameshatakiwa kwa makosa ya kukwepa kodi, mwendesha mashtaka wa Ujerumani amethibitisha.
Imegundulika kwamba mnamo April mwaka huu, Uli, 61, alishindwa kulipa kodi ya kodi akaunti yake iliyopo nchini Switzerland mnamo mwezi January, na sasa imethibitika ameshtakiwa kwa makosa ya kukwepa kodi.
"Mwendesha mashataka wa jiji la Munich II amekamilisha uchunguzi," taarifa rasmi ilisema.
"Mahakama ya makosa ya jinai ya mkoa wa Munich II sasa inasubiriwa kuamua kukubali au kukataa mashtaka hayo."
Msemaji wa klabu ya Bayern Markus Horwick aliiambia SZ kuhusu issue hiyo: "Hatutosema kitu chochote kuhusu suala hili."
No comments:
Post a Comment