WANATAALUMA WA KIISLAM WATAMBUA MCHANGO WA WASOMI NA TAASISI.
Dada
ambaye ni mwanasheria Bi Shamim Daudi akichangia maoni yake wakati wa
Kongamano la wanataaluma wa Kiislam Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan 1434 ambapo wanataaluma, wanazuoni na taasisi zilitunukiwa zawadi na Pesa taslim.
Wawakilishi
wa Taasisi na makundi yalizotunukiwa Zawadi za kutambua Juhudi
zilizotukuka katika kusukuma mbele juhudi mbali mbali za jamii ya
Kitanzania.
Ndugu
Ramadhani Sanze Katibu Mkuu wa Baraza Kuu akifurahia baada ya kupokea
zawadi kwa kuwakilisha taasisi za kiislam zilizoleta athari nzuri
kiuchumi ndani ya Jamii ambayo ilikabidhiwa kwa SACCOS iliyochini ya
Baraza Kuu iitwayo Kutayba ambayo hutoa Mikopo isiyo na Riba.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Islamic Foundation akipokea Zawadi ya Kuwakilisha Taasisi
zote za Kiislam zilizo mstali wa Mbele Kuelimisha Jamii kufahamu uislam
na kujenga Taifa lenye amani na Utulivu.
Mtafiti
na Mtunzi Maarufu wa Historia za Kijamii Sheikh Mohamed Said (Wa Kwanza
Kushoto) ni Mmoja wa Wanataaluma Wakongwe Waislam waliopewa zawadi na
Umoja wa Wanataaluma wa Kiislam Tanzania kama miongoni mwa wasomi
waliojitahidi Kuisadia Jamii wa Watanzania Kufahamu Historia sahihi ya
Tanganyika.
Dada
Riziki Shahari akikabidhi zawadi ya uwakilishi wa wanawake wa kiislam
wa kutolea mfano katika kuhamasisha jamii katika kujenga jamii yenye Maadili na Manufaa kwa Mustakabali ya Taifa.
Sheikh
Jabir Katura wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Mwanza (Wa kati kati)
alipokabidhiwa zawadi ya Kutambuliwa kama Miongoni Mwa Masheikh wenye
Kusimamia mambo ya dini kwa Haki na Kwa Manufaa ya Jamii. Wakimkabidhi
Zawadi hiyo Mwenyekiti wa Wanataaluma wa Kiislam Bw. Mussa Mziya
(Kushoto) Pamoja na Mwenyekiti wa Wanazuoni wa Kiislam Tanzania (Hay’at
Ulaamaa) Sheikh Suleiman Amran Kilemile.
Mwakilishi
wa Taasisi ya Islamic Help ya Uingereza Ndugu Shukuru Mohamed
akikabidhiwa zawadi ya Kutambua taasisi hiyo kwa Mchango wake juu ya
Watoto yatima katika Tanzania.
No comments:
Post a Comment