Pages

Saturday, July 13, 2013

Juninho

MCHAWI WA MIPIRA ILIYOKUFA JUNINHO KUCHEZA BURE VASCO DA GAMA ILI ALIPWE MADENI YAKE YA NYUMA

Mchezaji wa zamani wa Brazil Juninho Pernambucano anatarajia kucheza bure baada ya kurudi kwenye timu ya Vasco de Gama.

Kiungo huyo mwenye miaka 38, ambaye aliwahi kuitumikia klabu hiyo katika vipindi viwili tofauti, anajiandaa kurudi kwa kipindi cha tatu kwenye klabu hiyo yenye maskani yake ya Rio De Jeneiro ambapo hatopata mshahara.


Badala yake, nyota huyo wa zamani wa Lyon ameripotiwa atapokea malipo ya madeni yake yote ya zamani anayoidai klabu hiyo.  


Inaeleweka kwamba Juninho atarudi kujiunga na klabu hiyo ya Brazil kwa miezi sita kabla ya kutundika daluga zake. 

Mapema mwezi huu alimaliza mkataba wake na klabu ya MLS  New York Red Bulls baada ya miezi saba, ambapo alikatisha mkataba wake akitoa sababu binafsi ndio zilizosababisha

No comments:

Post a Comment