Pages

Tuesday, October 1, 2013

Haya ndio Maswali muhimu ya kujiuliza kila siku.


Kujiuliza maswali ni moja ya namna ya kutaka kupata majibu. Ni busara kama kila siku angalau kwa dakika chache utajiuliza maswali ya kukujenga kifikra na kupanua wigo wa manufaa katika maisha yako. Majibu ya maswali haya yenye tija yatakupa nuru na kukubadilisha kuwa mtu bora zaidi.
''Watch this video explaining the most important questions you can ask yourself throughout your day.''
 
1. Ni kitu gani kizuri ulichofurahia siku ya leo?
-Moja ya sifa ya maisha mazuri ni kufurahia kile unachofanya kila siku. Itakuwa ni faraja kubwa sana kutambua chochote kizuri kilichotokea kwako au kwa namna moja au nyingine kimekufurahisha kwa siku ya leo. Utakapo jua uzuri wa kitu ndio mwanzo wa kujua ni kwa kiasi gani maisha ni ya kipekee kwako.
 2. Umefanya kitu gani bora siku ya leo?
-Ni vyema ujue umejifunza nini leo? Ni makosa gani uliyofanya kwa siku ya jana na leo umeyarudia? Je una mpango gani wa kujirekebisha au kuepuka kurudia makosa yanayokusogeza mbali na ndoto zako? Kila siku jaribu kuboresha maisha yako ya sasa na ya baadae iwe kiafya ,kiuchumi au kitabia.
 
3.Ni jambo gani muhimu kwako unalotaka kukamilisha siku ya kesho?
-Kabla hujaanza siku nyingine hakikisha umeshajua siku inayofuata utafanya nini. Chukua karatasi na kalamu orodhesha mambo yote utakayofanya siku ya kesho kisha weka ratiba yako sehemu ambayo unaweza ukaiona kirahisi kila utakapo ihitaji. Kumbuka kuzingatia na kutekeleza kila jambo lililomuhimu kwako.
 4.Unategemea kufanya kitu gani kipya au tofauti  siku ya kesho?
-Maisha ni safari ndefu yenye miujiza ya mafanikio inayotokea kila siku kwa watu wanaofanya bidii kwa kile wanachotafuta. Milango ya bahati hufunguka kwa wale wanaojaribu mambo tofauti katika maisha yao. Mabadiliko yanaweza kuwa ya kibiashara, kijamii au kisiasa anza leo kwa kile unachoona unataka kiwe sawa. Mfano: Siku ya kesho unataka kubadilisha mlo wako mchana kwa kula chakula tofauti na siku nyingine. Au kesho unataka kubadilisha aina ya mazoezi ya mwili badala ya kunyoosha viungo vyako vya mwili unaamua kukimbia mchakachaka. Hivi ndivyo tunavyotakiwa tubadilike.
   
5.Ni watu gani muhimu sana kwako? Umepanga kuwafanyia nini ili kuimarisha mahusiano baina yako na wao?
-Thamini watu wote lakini wapende zaidi waliokaribu na wewe katika maisha yako kama vile wazazi, watoto au mpenzi wako. Je umeonyesha kuwa unawajali na kuwapenda? Wakati mwingine huwa tunatingwa na mambo mengi na kusahau watu waliomuhimu kwetu. Kila unapojiuliza swali hili litakufanya uwakumbuke wote waliomujimu kwako. Jijengee mazoea na mahusiano mazuri na washirika wako kwa kushirikiana nao vizuri nao watakupenda.
Maswali haya ni ya msingi sana, kila unapojiuliza na kupata majibu ya maswali haya nina imani yataleta athari ya kimaendeleo katika maisha yako. Jiulize leo hakika mafanikio yatakuwa karibu yako.
 


Pima maendeleo yako kwa kujiuliza maswali haya....



Kwa mtu makini na hodari anayependa kujiendeleza iwe kiimani, kimahusiano, kiafya, kikazi au kitaaluma hujiwekea malengo na kumbukumbu ya mafanikio yake  kila wakati anapopiga hatua.
Yafuatayo ni maswali kadhaa yatakayokusaidia kutafakari na kupima mafanikio au udhaifu wako ikiwa unadhumuni la kuwa mtu bora zaidi.
Jiulize maswali yafuatayo...

1. Umefanikisha nini katika miezi mitatu (3) iliyopita, na kwanini kitu hicho kilikuwa na maana kubwa kwako?
 2. Je ulipata changamoto gani katika kufanikisha malengo yako ya nyuma? Mambo gani yalikukwaza? Utafanya nini kusonga mbele?


3. Ni maeneo gani katika maisha yako yanayohitaji mkazo au umakini zaidi?
Mfano: Je unahitaji kukazia katika  uchumi wako, afya yako, kazi yako, familia yako au uhusiano wako na ndugu, jamaa au rafiki zako.. Utafanyaje ili kuweka mambo sawa?

4. Je ni zipi ndoto zako au matumaini yako? Je umeweka mikakati mizuri ya kupata utakacho?
5. Je ni maeneo gani ya kazi au shughuli zako unataka kubadilisha au kuboresha zaidi ili kuongeza tija na mafanikio yako ya baadae?

6. Je ni mafanikio ya kiasi gani unayofurahi kuyapata na kutoa msaada kwa wengine?
Itakuwa ni vyema kila baada ya miezi mitatu (3) upime maendeleo ya maisha yako. Weka jitihada na mafanikio yako katika darubini kulingana na mategemeo yako. Kisha endelea kuongeza bidii na kuwa na imani utafanikiwa, Unaweza pia ukawa na kitabu rasmi kwaajili ya kuweka kumbukumbu za maendeleo yako. Kila hatua ndogo unayopiga rekodi kwenye kitabu, hii itakusaidia kuona ni jinsi gani upo karibu au mbali na malengo yako. Kumbuka usisahau kujipongeza kwa kila mafanikio madogo au makubwa unayoyapata.

Haya ndiyo Mambo (18) ya kuimarisha MAISHA yako

 
Ni vigumu kuona maisha yapo sawa ikiwa una mtazamo tofauti na ukweli wa ulimwengu ulivyo. Zaidi ni kwamba licha ya kuwa utafikiria ufikiriavyo mwishowe utaishia kuona ulimwengu ndivyo ulivyo. Maisha ni mjumuiko wa kila aina ya mambo kuna mazuri na mabaya pia. Kujikumbusha mambo yaletayo amani, faraja na matumaini katika maisha yako ni kitu cha msingi sana kwakuwa sisi binadamu ni watu wa kusahau. Ili uweze kudumisha haiba yako ni vizuri kila siku kujikumbusha mambo haya kuimarisha mahusiano yako na watu wengine, tabia na ushirikiano wako ndani ya familia, jamii au jumuiya unayohusika.

1.Ongea na watu wote, usifikirie sana nini wanachokiwaza juu yako.

2. Kuwa rafiki mzuri kwa watu wanaokuzunguka, tabasamu na uso wa bashasha hufanya siku yako kuwa nzuri.

3. Thamini urafiki wenu na marafiki zako, sio lazima ujenge urafiki na kila mtu lakini waonyeshe kuwa unawajali hao wachache ulionao.

4. Fanya na fuata kile moyo wako unachopenda ilimradi ni kizuri huna sababu ya kuwa na mashaka nacho.

5. Ishi kwa kuona hakuna mtu au kitu kilichokamilika. Ona makosa ni moja ya mapungufu yanayotufundisha nini tujirekebishe.

6. Sahau chochote kibaya watu wanachofikiri au kudhani kuhusu wewe.

7. Linda afya yako kwa kula vyakula bora, furahia kunywa na kula vyote vizuri na vitamu vijengavyo afya bora.

8. Fanya maozezi mara kwa mara, yatakusaidia kuweka mwili wako sawa wakati wote.

9. Kuwa mkweli kwako mwenyewe kwani unajua nini unapenda na nini hupendi. Usimfanyie kitu kibaya mtu mwingine usichokipenda na usiwe muongo kwa watu.

10. Ni sawa wakati mwingine kukereka au kukasirika juu ya kitu fulani, chunga usiwaumize wengine.

11. Omba msamaha pale unapoona umemkosea mtu. Jenga amani na upendo kati yenu ipo siku utakuwa na shida yako naye atakusaidia.

12. Usijiwekee ugumu kuelewa kitu, jifunze mambo mengi yatakusaidia kuelewa mazingira unayoishi vizuri.

13. Jifunze kutumia teknolojia vizuri na kwa tija. Vitu kama simu za mkononi, magari, computer na vingine vingi vipo kwaajili ya kurahisisha maisha.

14. Jifunze kupika kama hujui. Chakula ni lazima ule, ukijua kupika utaweza kuwa huru kupika mwenyewe chakula upendacho kwa wakati wowote. 

15. Kuwa na malengo na maisha yako, ni njia ya pekee ya kukusogeza karibu na yale yote utakayo.

16. Fanya yale yote upendayo ni namna moja wapo ya kufurahia maisha uliyonayo.

17. Usiwe na hofu juu ya chochote ambacho bado hakijatokea. Asilimia kubwa ya mambo tunayokuwa na wasiwasi nayo huwa mazuri tu.

18. Jaribu kufanya mambo tofauti, ni namna ya kugundua vitu vikubwa na vizuri zaidi.

MADHARA MA 5 YA KUTUMIA PAMBA KUSAFISHIA MASIKIO/ EAR STICK

 
 
1. Kwanza husukuma ndani zaidi uchafu
 sikioni(ear wax),ule utando unaotoka ndani
ya sikio.
Unapochokonoa sikio kwa pamba huupeleka
uchafu kuingia ndani zaidi ya sikio, hii
husababisha vijidudu kushambulia kuta za
ndani ya sikio na ngoma ya sikio, hupelekea
mtu kutosikia vizuri.

2. Pia kutumia pamba kusafishia sikio
huatarisha kutokwa damu masikioni.
Unaposukuma ndani zaidi pamba kwenye
kuta za sikio ni ngozi laini, unaweza kuona
viti damu kwenye pamba, hii hutokana na
pamba kukwangua kuta za sikio lako.

3. Kutoka maji maji yanayowasha au usaha
sikio.
Hizi pamba huweza kubakia sikioni na ikikaa
kwa muda mrefu itakuwa inazuia uchafu wa
sikio kutoka,pia kuharibu ngoma ya sikio,
huu
utando unaotoka sikioni kazi yake kulinda
sikio lisishambuliwe na vijidudu(bacter ia) na
uchafu mwingine unaoingia sikioni kama
vumbi, pamba ikiziba huchafu hautoki
kuweza kuoza na kutoa maji maji(usaha) na
sikio kuwasha.

4. Kuharibu kuta za ndani zaidi ya sikio.
Ni mara ngapi umeingiza pamba mpaka
mwisho ndani kabisa ya sikio, na hapo
ikigusa ndani zaidi mwisho tundu la sikio
karibia na ngoma ya sikio utasikia maumivu,
hii ni kwasababu ya pamba kuumiza kuta za
ndani ya sikio mpaka kwenye ngoma ya sikio
inaweza kuchanika hii ni hatari zaidi.

5. Kukwaruza kuta za siko.
Baada tu ya kutumia pamba kusafisha sikio
utasikia muwasho ndani ya sikio hii
inamaanisha umekwaruza kuta za sikio na
pamba zinazotumika ni kavu, apo mtu
huendelea kusafisha ili mradi asisikie
muwasho matokeo yake ni kukwaruza zaidi
kuta za sikio hii naweza kusababisha
vidonda
ndani ya sikio.

N.B- Ushauri, ni vizuri ukangoja ushafu au
utando wa sikio ukatoka wenyewe nje apo
ukautoa kirahisi zaidi kuliko kulichokonoa
sikio, ukishindwa hii njia tumia kipande cha
nguo safi kiloweshe maji na taratibu usafishe
sikio lako, kwa watoto usimwingize pamba
masikioni kama umeshindwa kumtoa utando
wa sikioni kwa njia niliyoshauri apo juu ni
bora humpeleke hospitali kuna njia salama
zaidi (bulb syringe) hii hufanya kwenye
mahospitali chini ya uangalizi maalumu wa daktari!!