Pages

Sunday, July 28, 2013

Hii ndiyo sababu kwanini nilirudi brazil - Ronaldinho



RONALDINHO ATHIBITSHA KUWA ANATISHA NA KUIWEZESHA KLABU YAKE KUWA MABINGWA WA BARA LA AMERIKA YA KUSINI


Kombe la Dunia, Kombe la Mabara, Kombe la Mabingwa wa ulaya, Copa America, Ubingwa wa Serie A na makombe mawili ya La Liga.
Kuna vikombe vichache sana ambavyo Ronaldinho hajashinda bado katika maisha yake ya soka lakini usiku wa jana aliongeza idadi ya makombe makubwa ambayo amewahi kushinda - baada ya kuvaa medali ya kombe la mabingwa wa America ya kusini Copa Liberatadores.


Mbrazili huyo ambaye alijiunga na Atletico Mineiro kiangazi kilichopita na mpaka sasa ameshajishindia tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Brazil - akasaidia klabu yake kushinda ubingwa wa kwanza wa America ya Kusini.

Timu anayochezea Ronaldinho ilifungwa 2-0 katika mechi ya kwanza lakini waliweza kufanya 'comeback' katika mechi ya pili kwa kushinda 2-0 na kusababisha mechi kwenda hatua ya mikwaju ya penati na hatimaye wakashinda 4-2.

Pamoja na kiungo huyo mwenye miaka 33 kushinda makombe mengi na vilabu vyake, pia ana utajiri wa tuzo binafsi akiwa nazo 23 mpaka sasa 

Mshambuliaji alikuwa na wakati mzuri akivichezea vilabu kama FC Barcelona na AC Milan barani ulaya ambapo alishinda navyo ubingwa wa ulaya na makombe ya ndani.

Lakini ubingwa wa Copa Liberatadores ndio kombe kubwa zaidi kwa ngazi ya klabu barani America ya Kusini na kombe hili ni  maalum sana kwa mchezaji huyu bora wa dunia wa zamani 
 
 
'Hii ndio sababu kwanini nilirudi Brazil,' Ronaldinho alisema. 'Muda mfupi uliopita baadhi yawatu walikuwa wakisema kwamba nimeisha, lakini tumeonyesha hilo jambo sio kweli.'





No comments:

Post a Comment