Pages

Thursday, July 18, 2013

Maurinho amgeukia Higuain

Baada ya Rooney, Mourinho anamtaka Guonzalo Higuain

Higuain akiwa na wachezaji wenzie wa Real Madrid.
Baada ya kocha Jose Mourinho ku-make headlines jana kwa kauli yake ambayo alithibitisha kuwa anamtaka Wayne Rooney toka Manchester United baada ya taarifa kuvuja kuwa Chelsea imepeleka ofa ya paundi milioni 10, mshambuliaji  wa kimataifa toka Argentina Guonzalo Higuain ambaye kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na usajili wa klabu ya Arsenal ametoka na kauli ambayo itawachanganya wengi .
Striker huyo mwenye umri wa miaka 25 amedai kuwa kocha huyo Mreno (Mourinho) amempa ahadi kuwa atamnunua na kumfanya kuwa mchezaji wa Chelsea ikiwa ni kauli ambayo haitawafurahisha mashabiki wengi wa Arsenal ambao wamekuwa wakingoja kwa hamu uthibitisho wa usajili wa mchezaji huyo bila mafanikio. Higuain akiwa na wachezaji wenzie wa Real Madrid.
Zaidi ya hapo kauli hii pia itashangaza wengi kutokana na uhusiano mbaya ambao Mourinho na Guonzalo walikuwa nao wakati wakiwa Madrid ambapo Mourinho aliwahi kutamka kuwa Muargentina huyo ndio mchezaji mvivu kuliko wote aliowahi kuwafundisha.
Awali makubaliano ya msingi kati ya Arsenal na Madrid pamoja na wawakilishi wa Gonzalo Higuain yalifanyika ambapo ilikuwa kitendo cha muda kabla ya Arsenal kuthibitisha kumnunua mchezaji huyo, hata hivyo hali ilibadilika baada ya kocha Carlo Ancelotti kuingia Real Madrid ambapo alisema kuwa anataka kukaa na kikosi chote cha Madrid kabla ya kufanya maamuzi ya kuongeza au kupunguza wachezaji

No comments:

Post a Comment