WAFUASI WA MORSI WAANDAMANA CAIRO
Wafuasi wa rais wa Misri
aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi wamefanya maandamano makubwa
mjini Cairo, huku waumini wa dini ya Kiislamu wakiadhimsiha Ijumaa ya
kwanza tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Wafuasi wa kiongozi huyo wa vugu vugu la Muslim
Brotherhood walijikusanya Mashariki mwa mji huo, kushinikiza utawala wa
kijeshi kumrejesha madarakani kiongozi wao.Wapinzani wa rais huyo wa zamani ambao waliandamana hadi rais huyo akaondolewa madarakani na jeshi watakusanyika katika medani ya Tahrir.
Watu kadhaa wameuawa kwenye ghasia zilizotokea tangu Morsi alipoondolewa.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo, Jim Muir anasema vuguvugu la Muslim Brotherhood huenda liliwatenga raia wengi wakati wa utawala wa Morsi, lakini bado raia wengi wa nchi hiyo hawataki jeshi kuingilia masuala ya siasa.
No comments:
Post a Comment