Pages

Saturday, June 22, 2013

Kutoka MOAT

Makampuni ya simu kupandisha gharama Julai 1

Kufuatia kuongezwa kwa kodi katika huduma za simu za mkononi , gharama za huduma hizo zinatajiwa pia kuongezeka kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa jijini Dar es salaam na Umoja wa Makampuni ya Simu za Mkononi Tanzania – MOAT imesema pendekezo la serikali la kuweka kodi ya 14.5 kwenye huduma za simu za mkononi hazotoweza kukwepesha kupanda kwa gharama za simu kwa watumiaji.

MOAT inasema awali kodi ilikuwa ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya mawasiliano ya simu na kwmaba ongezeko la kufiikia asilimia 14.5 tofauti na nchi za jirani Kenya na Uganda ambazo zimeendelea kutoza viwango vya ushuru vya asilimia 10 na 12.5 tu ni mzigo kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi.

Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2013 unaainisha, huduma za mawasiliano kuwa ni; “huduma yoyote ya maelezo inayotolewa na makampuni ya mawasiliano ya simu kwa njia ya mawasiliano kwa kutoa au kupokea sauti, maandishi, na picha au taarifa ya aina yoyote kupitia mfumo wa kielektronikia.”Imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel.

MOAT imesema eneo mojawapo litakaloathirika ni huduma za Intaneti eneo amablo linahitaji kuwekewa mikakati ya kulikuza kutokana na umuhimu wake katika maisha ya sasa kiuchumi na kijamii na wala sio kulizorotesha kwa kusababisha ongezeko la gharama na hivyo kuendelea kuwa na kiwango cha cha matumizi kilinganishwa na baadhi ya nchi nyengine zikiwemo za Afrika Mashariki.

“Hatua hii ya kuongeza kodi itakwenda kinyume na mipango iliyopo yenye lengo la kuibadili jamii kwa kuipatia maarifa ya msingi kupitia huduma ya intaneti sambamba na mawasiliano ya simu.”

Kwa mujibu wa MOAT, Tanzania ni kati ya nchi zenye kiwango cha chini ya matumizi ya huduma ya mtandao wa intaneti katika bara la Afrika ambapo watumiaji wa huduma hiyo ni asilimia 10 pekee ikilinganishwa na nchi jirani ya Kenya ambayo ina zaidi ya watumiaji asilimia 40.

Aidha, MOAT imeongeza kuwa, “mawasiliano ya simu si anasa bali ni huduma muhimu katika Tanzania ya leo, sasa tunawezaaje kuwatozakodi mara kwa mara watu hao hao ambao wanaitegemea huduma hiyo ili kuboresha maisha yao? Ilihoji taarifa hiyo ya MOAT.

Taarifa hiyo  imeendelea kusema kuwa kwa tozo la kodi ya mapato ya  asilimia 35 kwenye sekta hiyo ya mawasiliano ya simu linatosha kiasi ya kwamba sekta hiyo isngeweza kubeba mzigo zaidi wa ongezeko jingine.
Hivi sasa, upanuzi wa mawasiliano na miundombinu vijijini ndiyo kipaumbele cha sekta nzima. Tunaamini hapa ndipo ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya simu itakapoonekana katika miaka ijayo. Ongezeko lolote la kodi litazorotesha uwezo wetu wa kutanua huduma zetu za mawasiliano na miundombinu maeneo ya vijijini, imesema MOAT.

“Tunaelewa kuwa serikali inayafanya haya yote ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya kusaidia kwenye huduma za jamii katika maeneo muhimu. Ni bahati mbaya kwamba sekta ya huduma ya mawasiliano ya simu inaendelea kubeba mzigo mkubwa wa ongezeko hili ambapo wateja watalazimika kuubeba mzigo wa ongezeko hilo,” ilihitimisha taarifa hiyo ya MOAT.

Friday, June 21, 2013

Chadema


SIRI YAFICHUKA.... CHADEMA WATHIBITISHA KUTUMIA MITAMBO MAALUM YA DVR KUMNASA MLIPUAJI WA BOMU LA ARUSHA



Imethibitika kwamba technology ya mawasiliano hivi sasa imekua kwa kasi ya ajabu sana, kiasi chakufikia kuwa kumbe siyo lazima tutegemee camera za waandishi wa habari kuchukua matukio.

Ni kwamba chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kwenye mkutano wake wa mwisho licha ya kutumia SATELLITE kurekodi mikutano yake, imethibitika kuwa chama hicho kilitumia mtambo maalum wa mawasiliano kurekodi mkutano wake wa mwisho katika uwanja wa soweto Arusha. Mtambo huo ambao unauwezo wa kurekodi matukio kwa masaa.. 72 mfululizo bila kuhitaji chaji, ulifungwa sehemu maalum ili kuweza kunasa matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye mkutano.

Mtambo huo ulisaidia kunasa tukio la mlipuko wa bomu na matumizi ya risasi kwenye mkutano kuwapiga raia, ambapo ulionyesha askari polisi aliyesimama pembeni ya nguzo ya umeme karibu na mfereji ulio mkabala na round about iliyo karibu na soweto garden akiwapiga risasi watu waliokuwa wanamkimbiza mtu aliyevaa suruali ya jeans aliyekimbia nakuingia kwenye gari ya polisi na kuondoka kwa kasi kwenye eneo la tukio. Mtambo pia uliweza kuonyesha gari ya blue landcruiser iliyoweza kui escort gari ambayo amepanda tule mtu aliyekuwa anakimbizwa.

Ule mtambo ambao una uwezo wa kurekodi matukio kwa around 360 degree angle uliweza kuonyesha tukio la watu wanaosadikiwa kuwa maaskari kufika kwenye eneo la tukio hasa kwenye gari la matangazo la chadema majira ya usiku, na kuweza kuzurura pale bila kuonyesha kwa kina walichokuwa wanakifanya pale.

video inaonyesha ule mtambo ulizima wenyewe saa moja na madakika asubuhi ya siku ya pili.

Kwa ujumla mtambo una taarifa nyeti za kuweza kusaidia kwa ushahidi wa tukio hili ambalo limegharimu maisha wa watu wasiokuwa na hatia. Muda utakapofika nadhani kwa idhini ya mwenyekiti wa chama kila kitu kitawekwa wazi

Habari za Michezo

MMOJA AFARIKI KATIKA MAANDAMANO  BRAZIL.

Raisi wa Brazil, Dilma Rousseff ameitisha mkutano wa dharura leo ikiwa ni siku moja baada ya muandamanaji kuuwawa na wengine zaidi ya milioni 1.25 wakiendelea kuandamana nchi nzima wakidai huduma nzuri kwa jamii. Pilikapilika hizo za uandamanaji ambazo mara nyingine zinaleta vurugu kubwa, zinafanyika wakati nchi hiyo iikiwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Shirikisho inayoendelea ambayo huchezwa mwaka mmoja kabla ya Kombe la Dunia. Raia wengi wa Brazil wamekuwa wakigadhabika juu ya gharama kubwa za maandalizi zilizotumika kwa ajili ya kuandaa na Kombe la Dunia 2014 na michuano ya olimpiki kipindi cha kiangazi itakayofanyika jijini Rio de Janeiro 2016.  Jijini Rio polisi wamekuwa wakipambana na waandamanaji hao ambao hujikusanya karibu na Uwanja wa Maracana ambapo wamekuwa wakilazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto ili kuwatawanya.
 

PIRLO KUIKOSA BRAZIL.

Kiungo mahiri wa kimataifa wa Italia, Andrea Pirlo anatarajiwa kukosa mchezo wa mwisho wa kundi A dhidi ya wenyeji Brazil kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kupata majeraha ya msuli katika mguu wake wa kulia. Kocha wa viungo wa nchi hiyo, Enrico Castellacci amesema anamatumaini Pirlo anaweza kurejea katika mechi ya nusu fainali lakini ukijumuisha na kukosekana kwa Daniele De Rossi ambaye naye pia atakosa mchezo wa mwishoni itabidi kocha wa timu hiyo Cesar Prandelli abadili kikosi chake. Italia ilitinga hatua ya nusu fainali baada ya kuibugiza Japan ka mabao 4-3 na kufikisha alama sawa na Brazil katika kundi lao ambapo mechi ya mwisho ndio itakayoamua nani atasonga mbele kama mshindi wa kundi. Timu zote mbili itabidi zipange vikosi vyao kamili ili kutafuta ushindi na kuepuka kukutana na bingwa wa dunia Hispania katika hatua ya nusu fainali.

HISPANIA WAPORWA HOTELINI WAKATI WAKIWA KWENYE MECHI.

Vyombo vya habari nchini Hispania vimeripoti kuwa wachezaji sita wa timu ya taifa ya Hispania wameibiwa fedha zao katika vyumba walivyofikia katika hoteli moja jijini Recife wakati wanacheza mchezo wao ufunguzi wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Uruguay. Mojawapo ya wachezaji waliokumbwa na mkasa huo ni beki wa Barcelona, Gerard Pique ambaye aligundua kaibiwa wakati aliporejea chumbani kwake baada ya mchezo dhidi ya Uruguay ambao walishinda kwa mabao 2-1. Msemaji wa Shirikisho la Soka Dunia-FIFA, Pekka Odriozola alikiri kupata taarifa hizo lakini wameziachia mamlaka husika kushughulikia na kisha kuwaletea taarifa kamili. Hispania ambao wako kundi B jana wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa kishindi baada ya kuishindilia Tahiti kwa mabao 10-0 wakati wawakilishi pekee wa Afrika kwenye mashindano hayo walishindwa kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Uruguay.

MERCEDES WAFUNGIWA KUFANYA MAJARIBO MSIMU HUU.

Timu ya Marcedes imefungiwa kufanya majaribio kwa madereva wake chipukizi kwa mwaka huu pamoja na kupewa onyo kali kwa kosa la kufanyia majaribio magurudumu ya Pirelli kinyume cha utaratibu. Kampuni hiyo ya magurudumu ya Pirelli nayo pia imepewa onyo kwa kutumia gari jipya linalotumiwa katika mashindano ya langalanga na dereva Lewis Hamilton katika majaribio ya siku tatu waliyofanya nchini Hispania mwezi uliopita. Kamati maalumu ya uchunguzi wa suala hilo iliyoundwa na Chama cha Kimataifa cha Langalanga-FIA kilichukua hatua hiyo baada ya kuwakuta Mercedes na hatia ya kutenda kosa hilo ambalo ni kinyume cha utaratibu wa mashindano hayo. Katika sheria za langalanga timu yoyote hairuhusiwi kufanya majaribio magurudumu kwa zaidi ya kilometa 1000 pindi msimu wa mshindano hayo unapoanza na hata wakifanya majaribio hayo hawapaswi kutumia gari zao mpya zinazotumika katika msimu husika.
 

Afya Yako

MACHUNGWA, ZABIBU HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA KIHARUSI? 

MACHUNGWA, ZABIBU HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA KIHARUSI?
 Utafiti mpya uliofanyika nchini Marekani  umesema ya kwamba kula machungwa na zabibu kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi (Stroke).
Utafiti huo uliangalia faida za matunda chachu(Citrus Fruit) pekee kwa  mara ya kwanza tofauti na tafiti nyingi ambazo tumezizoea zinazoangalia umuhimu wa matunda na mboga za majani kwa afya kiujumla.
Utafiti huu umehusisha maelfu ya wanawake wanaoshiriki katika tafiti ya manesi  Nurse’s Health Study lakini wataalamu wanaamini faida hizo  za machungwa na zabibu pia zinapatikana kwa wanaume.
Timu ya watafiti katika chuo cha Norwich Medical School katika Chuo Kikuu cha  East Anglia wamechunguza umuhimu wa kemikali aina ya flavonoids ambayo ni jamii ya antioxidant (kemikali zinauwa kemikali hatari za kwenye mwili) inayopatikana katika matunda, mboga za majani, chocolate nyeusi na wine nyekundu.
Utafiti huu ulifuatilia takwimu za miaka 14 za wanawake 69,222 ambao walikuwa wakishirki katika tafiti kwa kuandika kiwango chao cha kula matunda na mboga za majani kwa kila kipindi cha  miaka 4. Timu hiyo ya utafiti iliangalia uhusiano wa aina sita ya flavonoids – flavanones, anthocyanins, flavan-3-ols, flavonoid polymers, flavonols na flavones na hatari ya aina mbalimbali za kiharusi kama Ischaemic, Hemorrhagic na Total Stroke. Ilionekna wanawake waliokula kiwango kikubwa cha flavanones kwenye matunda chachu walikuwa na asilimia 19 ya uwezekano wa kupunguza kiharusi kulinganisha na wanawake ambao walikula kiwango kidogo cha matunda hayo.
Kiwango kikubwa cha flavanones kilikuwa 45mg kwa siku kulinganisha na kiwango kidogo cha  25mg kwa siku. Utafiti huu ulichapishwa katika jarida la Medical Journal Stroke umesema flavanones hupatikana kwa asilimia 82 kwenye machungwa na juisi ya machungwa na hupatikana kwa asilimia 14 kwenye zabibu na juisi ya zabibu. Hata hivyo watafiti hao wamesema kwa wale wenye kusudio la kuongeza kiwango kikubwa cha flavanones itawalazimu kula tunda la chungwa kwa wingi na si juisi za machungwa zinazotengenezwa kiwandani kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kinachopatikana katika juisi hizo za viwandani.
Professa Aedin Cassidy wa masuala ya lishe bora (nutrition) na ambaye alikuwa kiongozi wa utafiti huo amesema “kula kwa wingi kwa matunda, mboga za majani, na hasa Vitamin C uhusishwa na kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi”. Flavanones hutoa kinga dhidhi ya kiharusi kutokana na kuongeza ufanisi wa mishipa ya damu kwenye ubongo na kutokana na kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi mwilini (Anti-inflammatory effect).
Utafiti uliofanyika hapo awali ulionyesha ya kwamba ulaji wa matunda chachu na juisi yake na si matunda ya aina nyingine yoyote hupunguza uwezekano wa kupata  kiharusi aina ya Ischaemic Stroke na kuvuja damu kwenye ubongo (Intracerebral Haemorrhage).
MACHUNGWA, ZABIBU HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA KIHARUSI?














Utafiti mwingine uliofanyika kipindi cha nyuma ulionyesha hakuna uhusiano wowote wa matunda ya njano na machungwa katika kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi lakini ulionyesha ya kwamba kuna uhusiano wa zabibu na mapeasi wa kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi.
Katika utafiti mwingine uliofanyika nchini Sweden umeonyesha ya kwamba wanawake ambao walikula  kiwango kikubwa chaantioxidant karibia asilimia 50 kutoka kwenye matunda na mboga za majani, ni wachache tu kati yao waliopata kiharusi ikilinganishwa na wanawake ambao walikuwa na kiwango kidogo cha antioxidant.
Matokeo ya utafiti huu yasiwafanye watu kuacha kula matunda ya aina nyingine pamoja na mboga za majani kwani nayo yana faida kubwa katika mwili wa binadamu.
Kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi inawezekana kama mtu atakula lishe bora iliyo na virutubisho vyote muhimu, kula matunda na mboga za majani kwa wingi, kufanya mazoezi mara kwa mara, kupunguza kiwango cha ulaji chumvi (kwani watu wenye asili ya Kiafrika wana kiashiria cha asili kinachojulikana kama salt retention geneambacho hufanya kiwango kidogo cha matumizi ya chumvi mwilini kuonekana kama kiwango kikubwa na hivyo kuongeza hatari ya kupata kiharusi), kupunguza uzito (kuwa kwenye uzito unaotakikana kiafya  kulingana na umri na urefu wako), kupunguza kiwango cha matumizi ya mafuta katika chakula, kulala masaa ya  kutosha na kupunguza msongo wa mawazo.

News from White House

Obama kutembelea Africa


Obama kutembelea Africa

White  House imesema kuwa rais wa Marekani Barack Obama atakwenda Afrika  mwishoni mwa mwezi wa sita ambapo atazuru nchi tatu.
Katika taarifa Jumatatu jioni, White House  ilisema rais Obama na mke wake Michelle watakwenda Senegal,  Afrika Kusini na Tanzania mwishoni mwa Juni na mapema mwezi Julai.
Utawala wa rais Obama  unasema rais huyu wa Marekani atakutana na maafisa wa serikali, viongozi wa kibiashara, asasi za kiraia na makundi ya vijana.
Safari ya bw.Obama itaanza Juni 26 mpaka Julai 3 na inalenga kudhihirisha mahusiano ya karibu kati ya Marekani na nchi za Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara.
Rais Obama ambaye baba yake alizaliwa Kenya, alizuru Afrika  mara moja  katika muhula wake wa kwanza, alipotembelelea Ghana mwaka 2009.
Mkewe Michelle Obama pia amesafiri kwenda Afrika Kusini na Bostwana.

Kutoka NBA Championship


Washindi Wa 2013 NBA Championship




The Miami Heat have done it again.
Yes ni game 7 Chini ya King Lebron James, Miami Heat imeondoka na Points 95 Kwa 88 za San Antonio Spurs. Lebron ametoka na Point 37. Wade nae ametoka na point 23, rebounds 10 , Shane Battier ana points 18. Mpaka sasa Lebron ni Mshindi wa NBA Mara mbili na MVP Mara Mbili.


The Spurs wameongozwa na Tim Duncan akiwa na points 24, rebounds 12 na Kawhi Leonard ametoka na point 19 na rebounds 16 , Manu Ginobili ametoka na points 18.

BAN KI-MOON ALAANI SHERIA YA HABARI YA BURUNDI

Pierre
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameikosoa sheria mpya iliyopitishwa na serikali ya Burundi, ambayo amesema itaathiri uhuru wa vyombo vya habari.
Rais Pierre Nkurunziza, siku ya Jumanne aliridhia sheria hiyo, ambayo imekosolewa vikali na mashirika ya habari na yale ya haki za binaadamu.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky, alisema Katibu Mkuu Ban amesikitishwa na sheria hiyo, yenye vifungu vinavyoweza kukandamiza uhuru wa habari, huku akisisitiza kuwa haki ya uhuru ya kujieleza na sekta huru ya habari ni mambo muhimu kwa ustawi wa demokrasia.
Sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la Burundi mwezi April, inadhoofisha ulinzi wa vyanzo vya habari, inadhibiti kuripoti habari za uchunguzi, na inawataka waandishi wote kuwa na shahada ya Chuo Kikuu bila kujali uzoefu.
Pia inapiga marufuku kusambaza taarifa au nyaraka kuhusu mada za ulinzi au taarifa zinazochukuliwa kuwa propaganda za adui, au zinazoweza kuathiri uchumi wa Burundi.
Shirka la kutetea haki za waandishi la Reporters Without Boarders limeielezea sheria hiyo kuwa ni alama ya siku nyeusi kwa uhuru wa habari nchini Burundi.

Father of Africa

AFYA YA MANDELA SIO NZURI.


Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, angali katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa. Mandela amelazwa katika hospitali moja mjini Pretoria.
"mzee Mandela yuko hospitalini na hali yake bado haijabadilika.''
Maombi yakekuwa yakifanywa makanisani kote nchini Afrika Kusini kumuombea Mandela ambaye anatibiwa kwa ugonjwa wa mapafu.
Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi  ikiwa ni mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu.
Kwa mujibu wa duru za urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu.
Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.
Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais President Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba wakati huu anapougua.



Lakini mwandishi wa BBC mjini Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa kuna matumaini amdogo kuwa Mandela aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, huenda kupona.

Anasema kuwa wengi walipata matumani baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata nafuu.
Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.
Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999.
Alifungwa jela miaka 27 na anaaminika kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika machimbo ya mawe akiwa jela.
Habari na bbc swahili
 Dunia nzima inaungana kumuombea Mandela apone hata leo kumekuwepo na misa maalum ya kumuombea apone huko Afrika ya kusini.
Viva Mandela.....!!!