Makampuni ya simu kupandisha gharama Julai 1
Kufuatia
 kuongezwa kwa kodi katika huduma za simu za mkononi , gharama za huduma
 hizo zinatajiwa pia kuongezeka kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Taarifa
 ya pamoja iliyotolewa jijini Dar es salaam na Umoja wa Makampuni ya 
Simu za Mkononi Tanzania – MOAT imesema pendekezo la serikali la kuweka 
kodi ya 14.5 kwenye huduma za simu za mkononi hazotoweza kukwepesha 
kupanda kwa gharama za simu kwa watumiaji.
MOAT 
inasema awali kodi ilikuwa ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya 
mawasiliano ya simu na kwmaba ongezeko la kufiikia asilimia 14.5 tofauti
 na nchi za jirani Kenya na Uganda ambazo zimeendelea kutoza viwango vya
 ushuru vya asilimia 10 na 12.5 tu ni mzigo kwa watumiaji wa huduma za 
simu za mkononi.
Muswada
 wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2013 unaainisha, huduma za mawasiliano kuwa
 ni; “huduma yoyote ya maelezo inayotolewa na makampuni ya mawasiliano 
ya simu kwa njia ya mawasiliano kwa kutoa au kupokea sauti, maandishi, 
na picha au taarifa ya aina yoyote kupitia mfumo wa 
kielektronikia.”Imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Vodacom, Airtel, 
Tigo na Zantel.
MOAT 
imesema eneo mojawapo litakaloathirika ni huduma za Intaneti eneo amablo
 linahitaji kuwekewa mikakati ya kulikuza kutokana na umuhimu wake 
katika maisha ya sasa kiuchumi na kijamii na wala sio kulizorotesha kwa 
kusababisha ongezeko la gharama na hivyo kuendelea kuwa na kiwango cha 
cha matumizi kilinganishwa na baadhi ya nchi nyengine zikiwemo za Afrika
 Mashariki.
“Hatua
 hii ya kuongeza kodi itakwenda kinyume na mipango iliyopo yenye lengo 
la kuibadili jamii kwa kuipatia maarifa ya msingi kupitia huduma ya 
intaneti sambamba na mawasiliano ya simu.”
Kwa 
mujibu wa MOAT, Tanzania ni kati ya nchi zenye kiwango cha chini ya 
matumizi ya huduma ya mtandao wa intaneti katika bara la Afrika ambapo 
watumiaji wa huduma hiyo ni asilimia 10 pekee ikilinganishwa na nchi 
jirani ya Kenya ambayo ina zaidi ya watumiaji asilimia 40.
Aidha,
 MOAT imeongeza kuwa, “mawasiliano ya simu si anasa bali ni huduma 
muhimu katika Tanzania ya leo, sasa tunawezaaje kuwatozakodi mara kwa 
mara watu hao hao ambao wanaitegemea huduma hiyo ili kuboresha maisha 
yao? Ilihoji taarifa hiyo ya MOAT.
Taarifa
 hiyo  imeendelea kusema kuwa kwa tozo la kodi ya mapato ya  asilimia 35
 kwenye sekta hiyo ya mawasiliano ya simu linatosha kiasi ya kwamba 
sekta hiyo isngeweza kubeba mzigo zaidi wa ongezeko jingine.
Hivi 
sasa, upanuzi wa mawasiliano na miundombinu vijijini ndiyo kipaumbele 
cha sekta nzima. Tunaamini hapa ndipo ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya 
simu itakapoonekana katika miaka ijayo. Ongezeko lolote la kodi 
litazorotesha uwezo wetu wa kutanua huduma zetu za mawasiliano na 
miundombinu maeneo ya vijijini, imesema MOAT.
“Tunaelewa
 kuwa serikali inayafanya haya yote ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya
 kusaidia kwenye huduma za jamii katika maeneo muhimu. Ni bahati mbaya 
kwamba sekta ya huduma ya mawasiliano ya simu inaendelea kubeba mzigo 
mkubwa wa ongezeko hili ambapo wateja watalazimika kuubeba mzigo wa 
ongezeko hilo,” ilihitimisha taarifa hiyo ya MOAT.

No comments:
Post a Comment