MACHUNGWA, ZABIBU HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA KIHARUSI?

 Utafiti mpya uliofanyika nchini Marekani  umesema ya kwamba kula 
machungwa na zabibu kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi (Stroke).
Utafiti huo uliangalia faida za matunda chachu(Citrus Fruit) pekee
 kwa  mara ya kwanza tofauti na tafiti nyingi ambazo tumezizoea 
zinazoangalia umuhimu wa matunda na mboga za majani kwa afya kiujumla.
Utafiti huu umehusisha maelfu ya wanawake wanaoshiriki katika 
tafiti ya manesi  Nurse’s Health Study lakini wataalamu wanaamini faida 
hizo  za machungwa na zabibu pia zinapatikana kwa wanaume.
Timu ya watafiti katika chuo cha Norwich Medical School katika Chuo
 Kikuu cha  East Anglia wamechunguza umuhimu wa kemikali aina ya flavonoids ambayo ni jamii ya antioxidant (kemikali
 zinauwa kemikali hatari za kwenye mwili) inayopatikana katika matunda, 
mboga za majani, chocolate nyeusi na wine nyekundu.
Utafiti huu ulifuatilia takwimu za miaka 14 za wanawake 69,222 
ambao walikuwa wakishirki katika tafiti kwa kuandika kiwango chao cha 
kula matunda na mboga za majani kwa kila kipindi cha  miaka 4. Timu hiyo
 ya utafiti iliangalia uhusiano wa aina sita ya flavonoids – flavanones, anthocyanins, flavan-3-ols, flavonoid polymers, flavonols na flavones na hatari ya aina mbalimbali za kiharusi kama Ischaemic, Hemorrhagic na Total Stroke. Ilionekna wanawake waliokula kiwango kikubwa cha flavanones kwenye
 matunda chachu walikuwa na asilimia 19 ya uwezekano wa kupunguza 
kiharusi kulinganisha na wanawake ambao walikula kiwango kidogo cha 
matunda hayo.
Kiwango kikubwa cha flavanones kilikuwa 45mg kwa siku kulinganisha na kiwango kidogo cha  25mg kwa siku. Utafiti huu ulichapishwa katika jarida la Medical Journal Stroke umesema flavanones hupatikana
 kwa asilimia 82 kwenye machungwa na juisi ya machungwa na hupatikana 
kwa asilimia 14 kwenye zabibu na juisi ya zabibu. Hata hivyo watafiti 
hao wamesema kwa wale wenye kusudio la kuongeza kiwango kikubwa cha 
flavanones itawalazimu kula tunda la chungwa kwa wingi na si juisi za 
machungwa zinazotengenezwa kiwandani kutokana na kiwango kikubwa cha 
sukari kinachopatikana katika juisi hizo za viwandani.
Professa Aedin Cassidy wa masuala ya lishe bora (nutrition) na
 ambaye alikuwa kiongozi wa utafiti huo amesema “kula kwa wingi kwa 
matunda, mboga za majani, na hasa Vitamin C uhusishwa na kupunguza 
uwezekano wa kupata kiharusi”. Flavanones hutoa kinga dhidhi ya
 kiharusi kutokana na kuongeza ufanisi wa mishipa ya damu kwenye ubongo 
na kutokana na kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi mwilini (Anti-inflammatory effect).
Utafiti uliofanyika hapo awali ulionyesha ya kwamba ulaji wa 
matunda chachu na juisi yake na si matunda ya aina nyingine yoyote 
hupunguza uwezekano wa kupata  kiharusi aina ya Ischaemic Stroke na kuvuja damu kwenye ubongo (Intracerebral Haemorrhage).

Utafiti mwingine uliofanyika kipindi cha nyuma ulionyesha hakuna 
uhusiano wowote wa matunda ya njano na machungwa katika kupunguza 
uwezekano wa kupata kiharusi lakini ulionyesha ya kwamba kuna uhusiano 
wa zabibu na mapeasi wa kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi.
Katika utafiti mwingine uliofanyika nchini Sweden umeonyesha ya kwamba wanawake ambao walikula  kiwango kikubwa chaantioxidant karibia
 asilimia 50 kutoka kwenye matunda na mboga za majani, ni wachache tu 
kati yao waliopata kiharusi ikilinganishwa na wanawake ambao walikuwa na
 kiwango kidogo cha antioxidant.
Matokeo ya utafiti huu yasiwafanye watu kuacha kula matunda ya aina
 nyingine pamoja na mboga za majani kwani nayo yana faida kubwa katika 
mwili wa binadamu.
Kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi inawezekana kama mtu atakula
 lishe bora iliyo na virutubisho vyote muhimu, kula matunda na mboga za 
majani kwa wingi, kufanya mazoezi mara kwa mara, kupunguza kiwango cha 
ulaji chumvi (kwani watu wenye asili ya Kiafrika wana kiashiria cha 
asili kinachojulikana kama salt retention geneambacho hufanya 
kiwango kidogo cha matumizi ya chumvi mwilini kuonekana kama kiwango 
kikubwa na hivyo kuongeza hatari ya kupata kiharusi), kupunguza uzito 
(kuwa kwenye uzito unaotakikana kiafya  kulingana na umri na urefu 
wako), kupunguza kiwango cha matumizi ya mafuta katika chakula, kulala 
masaa ya  kutosha na kupunguza msongo wa mawazo.
No comments:
Post a Comment