AFYA YA MANDELA SIO NZURI.
Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, angali
katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa. Mandela amelazwa katika
hospitali moja mjini Pretoria.
"mzee Mandela yuko hospitalini na hali yake bado haijabadilika.''
Maombi yakekuwa yakifanywa makanisani kote nchini Afrika Kusini kumuombea Mandela ambaye anatibiwa kwa ugonjwa wa mapafu.
Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94,
alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi ikiwa ni mara ya tatu kulazwa
hospitalini mwaka huu.
Kwa mujibu wa duru za urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu.
Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.
Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais President
Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea
Madiba wakati huu anapougua.
Lakini mwandishi wa BBC mjini Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa
kuna matumaini amdogo kuwa Mandela aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa
ubaguzi wa rangi, huenda kupona.
Anasema kuwa wengi walipata matumani baada ya
bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa
anaendelea kupata nafuu.
Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.
Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999.
Alifungwa jela miaka 27 na anaaminika kuwahi
kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika
machimbo ya mawe akiwa jela.
Habari na bbc swahili
Dunia nzima inaungana kumuombea Mandela apone hata leo kumekuwepo na misa maalum ya kumuombea apone huko Afrika ya kusini.
Viva Mandela.....!!!
No comments:
Post a Comment