Kwa mtu makini na hodari anayependa kujiendeleza iwe
kiimani, kimahusiano, kiafya, kikazi au kitaaluma hujiwekea malengo na kumbukumbu
ya mafanikio yake kila wakati anapopiga
hatua.
Yafuatayo ni maswali kadhaa yatakayokusaidia kutafakari na
kupima mafanikio au udhaifu wako ikiwa unadhumuni la kuwa mtu bora zaidi.
Jiulize maswali yafuatayo...
1. Umefanikisha nini katika miezi mitatu (3) iliyopita, na
kwanini kitu hicho kilikuwa na maana kubwa kwako?
2. Je ulipata changamoto gani katika kufanikisha malengo yako
ya nyuma? Mambo gani yalikukwaza? Utafanya nini kusonga mbele?
3. Ni maeneo gani katika maisha yako yanayohitaji mkazo au
umakini zaidi?
Mfano: Je unahitaji kukazia katika uchumi wako, afya yako, kazi yako, familia
yako au uhusiano wako na ndugu, jamaa au rafiki zako.. Utafanyaje ili kuweka
mambo sawa?
4. Je ni zipi ndoto zako au matumaini yako? Je umeweka
mikakati mizuri ya kupata utakacho?
5. Je ni maeneo gani ya kazi au shughuli zako unataka
kubadilisha au kuboresha zaidi ili kuongeza tija na mafanikio yako ya baadae?
6. Je ni mafanikio ya kiasi gani unayofurahi kuyapata na
kutoa msaada kwa wengine?
Itakuwa ni vyema kila baada ya miezi mitatu (3) upime
maendeleo ya maisha yako. Weka jitihada na mafanikio yako katika darubini
kulingana na mategemeo yako. Kisha endelea kuongeza bidii na kuwa na imani
utafanikiwa, Unaweza pia ukawa na kitabu rasmi kwaajili ya kuweka kumbukumbu za
maendeleo yako. Kila hatua ndogo unayopiga rekodi kwenye kitabu, hii
itakusaidia kuona ni jinsi gani upo karibu au mbali na malengo yako. Kumbuka
usisahau kujipongeza kwa kila mafanikio madogo au makubwa unayoyapata.
No comments:
Post a Comment