Pages

Tuesday, October 1, 2013

Haya ndiyo Mambo (18) ya kuimarisha MAISHA yako

 
Ni vigumu kuona maisha yapo sawa ikiwa una mtazamo tofauti na ukweli wa ulimwengu ulivyo. Zaidi ni kwamba licha ya kuwa utafikiria ufikiriavyo mwishowe utaishia kuona ulimwengu ndivyo ulivyo. Maisha ni mjumuiko wa kila aina ya mambo kuna mazuri na mabaya pia. Kujikumbusha mambo yaletayo amani, faraja na matumaini katika maisha yako ni kitu cha msingi sana kwakuwa sisi binadamu ni watu wa kusahau. Ili uweze kudumisha haiba yako ni vizuri kila siku kujikumbusha mambo haya kuimarisha mahusiano yako na watu wengine, tabia na ushirikiano wako ndani ya familia, jamii au jumuiya unayohusika.

1.Ongea na watu wote, usifikirie sana nini wanachokiwaza juu yako.

2. Kuwa rafiki mzuri kwa watu wanaokuzunguka, tabasamu na uso wa bashasha hufanya siku yako kuwa nzuri.

3. Thamini urafiki wenu na marafiki zako, sio lazima ujenge urafiki na kila mtu lakini waonyeshe kuwa unawajali hao wachache ulionao.

4. Fanya na fuata kile moyo wako unachopenda ilimradi ni kizuri huna sababu ya kuwa na mashaka nacho.

5. Ishi kwa kuona hakuna mtu au kitu kilichokamilika. Ona makosa ni moja ya mapungufu yanayotufundisha nini tujirekebishe.

6. Sahau chochote kibaya watu wanachofikiri au kudhani kuhusu wewe.

7. Linda afya yako kwa kula vyakula bora, furahia kunywa na kula vyote vizuri na vitamu vijengavyo afya bora.

8. Fanya maozezi mara kwa mara, yatakusaidia kuweka mwili wako sawa wakati wote.

9. Kuwa mkweli kwako mwenyewe kwani unajua nini unapenda na nini hupendi. Usimfanyie kitu kibaya mtu mwingine usichokipenda na usiwe muongo kwa watu.

10. Ni sawa wakati mwingine kukereka au kukasirika juu ya kitu fulani, chunga usiwaumize wengine.

11. Omba msamaha pale unapoona umemkosea mtu. Jenga amani na upendo kati yenu ipo siku utakuwa na shida yako naye atakusaidia.

12. Usijiwekee ugumu kuelewa kitu, jifunze mambo mengi yatakusaidia kuelewa mazingira unayoishi vizuri.

13. Jifunze kutumia teknolojia vizuri na kwa tija. Vitu kama simu za mkononi, magari, computer na vingine vingi vipo kwaajili ya kurahisisha maisha.

14. Jifunze kupika kama hujui. Chakula ni lazima ule, ukijua kupika utaweza kuwa huru kupika mwenyewe chakula upendacho kwa wakati wowote. 

15. Kuwa na malengo na maisha yako, ni njia ya pekee ya kukusogeza karibu na yale yote utakayo.

16. Fanya yale yote upendayo ni namna moja wapo ya kufurahia maisha uliyonayo.

17. Usiwe na hofu juu ya chochote ambacho bado hakijatokea. Asilimia kubwa ya mambo tunayokuwa na wasiwasi nayo huwa mazuri tu.

18. Jaribu kufanya mambo tofauti, ni namna ya kugundua vitu vikubwa na vizuri zaidi.

No comments:

Post a Comment