Kujiuliza maswali ni moja ya namna ya kutaka kupata
majibu. Ni busara kama kila siku angalau kwa dakika chache utajiuliza
maswali
ya kukujenga kifikra na kupanua wigo wa manufaa katika maisha yako.
Majibu ya maswali haya yenye tija yatakupa nuru na kukubadilisha
kuwa mtu bora zaidi.
''Watch this video explaining the most important questions you can ask yourself throughout your day.''
1. Ni kitu gani
kizuri ulichofurahia siku ya leo?
-Moja ya sifa ya maisha mazuri ni kufurahia
kile unachofanya kila siku. Itakuwa ni faraja kubwa sana kutambua chochote
kizuri kilichotokea kwako au kwa namna moja au nyingine kimekufurahisha kwa
siku ya leo. Utakapo jua uzuri wa kitu ndio mwanzo wa kujua ni kwa kiasi gani maisha
ni ya kipekee kwako.
2. Umefanya kitu gani bora siku ya leo?
-Ni vyema ujue umejifunza nini leo? Ni
makosa gani uliyofanya kwa siku ya jana na leo umeyarudia? Je una mpango gani
wa kujirekebisha au kuepuka kurudia makosa yanayokusogeza mbali na ndoto zako?
Kila siku jaribu kuboresha maisha yako ya sasa na ya baadae iwe kiafya
,kiuchumi au kitabia.
3.Ni jambo gani muhimu kwako unalotaka
kukamilisha siku ya kesho?
-Kabla hujaanza siku nyingine hakikisha
umeshajua siku inayofuata utafanya nini. Chukua karatasi na kalamu orodhesha
mambo yote utakayofanya siku ya kesho kisha weka ratiba yako sehemu ambayo
unaweza ukaiona kirahisi kila utakapo ihitaji. Kumbuka kuzingatia na kutekeleza
kila jambo lililomuhimu kwako.
4.Unategemea kufanya kitu gani
kipya au tofauti siku ya kesho?
-Maisha ni safari ndefu yenye miujiza ya
mafanikio inayotokea kila siku kwa watu wanaofanya bidii kwa kile
wanachotafuta. Milango ya bahati hufunguka kwa wale wanaojaribu mambo tofauti
katika maisha yao. Mabadiliko yanaweza kuwa ya kibiashara, kijamii au kisiasa
anza leo kwa kile unachoona unataka kiwe sawa. Mfano: Siku ya kesho unataka
kubadilisha mlo wako mchana kwa kula chakula tofauti na siku nyingine. Au kesho
unataka kubadilisha aina ya mazoezi ya mwili badala ya kunyoosha viungo vyako
vya mwili unaamua kukimbia mchakachaka. Hivi ndivyo tunavyotakiwa tubadilike.
5.Ni watu gani muhimu sana kwako? Umepanga
kuwafanyia nini ili kuimarisha mahusiano baina yako na wao?
-Thamini watu wote lakini wapende zaidi
waliokaribu na wewe katika maisha yako kama vile wazazi, watoto au mpenzi wako.
Je umeonyesha kuwa unawajali na kuwapenda? Wakati mwingine huwa tunatingwa na
mambo mengi na kusahau watu waliomuhimu kwetu. Kila unapojiuliza swali hili
litakufanya uwakumbuke wote waliomujimu kwako. Jijengee mazoea na mahusiano
mazuri na washirika wako kwa kushirikiana nao vizuri nao watakupenda.
Maswali haya ni ya msingi sana, kila unapojiuliza
na kupata majibu ya maswali haya nina imani yataleta athari ya kimaendeleo
katika maisha yako. Jiulize leo hakika mafanikio yatakuwa karibu yako.
No comments:
Post a Comment