Pages

Friday, September 27, 2013

ETO'O: 'NISHAWAHI KUAPA KUTOCHEZA KWENYE TIMU INAYOFUNDISHWA NA MOURINHO - LEO HII KOCHA NI RAFIKI YANGU'


Samuel Eto'o amefunguka na kusema kwamba aliwahi kuapa kutokuja kucheza chini ya kocha Jose Mourinho.

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona alisema alikuwa na mahusiano yasiyoridhisha na na kocha wa kireno kabla ya hawajafanya kazi pamoja wakiwa Inter Milan, mahala ambapo walishinda vikombe vitatu kwa msimu mmoja. 

Eto'o ameungana tena na Mourinho wakati alipojiunga na Chelsea hivi karibuni akitokea klabu ya Anzhi Makhachkala kwa mkataba wa mwaka mmpja utaoisha wakati ujao wa kiangazi. 

Huu ulikuwa uhamisho ambao Eto'o mwanzoni asingeweza kukubaliana nao.

"Kabla hatujakutana kule Inter, Jose na mimi hatukujuana vizuri kwa ukaribu, hivyo mahusiano yetu hayakuwa yakieleweka," alikaririwa Eto'o alipohojiwa na gazeti la The Sun.

"Nadhani nilisema huko nyuma kwamba nisingekuja kuichezea klabu inayofundishwa na Jose.
“Lakini mungu anajua zaidi. Alitaka kunionyesha sikuwa sahihi na leo hii Jose ni rafiki yangu mkubwa, pia ni kocha wangu kwa mara nyingine tena."

No comments:

Post a Comment