Pages

Saturday, August 3, 2013

Usipitwe na mabadiliko haya ya Teknohama

 TEKNOHAMA SASA YAFIKIA KIWANGO HIKI

Maendeleo katika teknolojia ya mawasiliano hususani kwa vifaa vya matumizi ya mkononi kama vile simu yanazidi kuongezeka. Tunapoelekea ni kuwa watabaki watu wachache sana watakaotumia kompyuta za mezani (desktop computer), na hata laptop zinaelekea kupungua watumiaji, badala yake, watu wanaingia zaidi katika matumizi ya kompyuta ndogo na zinazohamishika toka sehemu moja kwenda nyingine. Katika makala yetu ya leo tunaangalia maendeleo makubwa tunayoyatarajia katika teknolojia ya mawasiliano:
Spidi kubwa ya mawasiliano:  Katika kurahisisha mawasiliano, wataalamu wamegundua teknolojia ya  LTE ( Long Term Evolution) ambayo pia huitwa 4G (4th Generation) ambayo ndio inayoelezwa kuwa tegemeo la kuifanya dunia iwe na mawasiliano ya kasi kubwa zaidi na kutokana na uwezo huo, basi vifaa vingi vitaweza kuunganishwa kupitia internet, na zaidi sana kuwezesha simu kufanya matumizi mengi ambayo yanafanyika sasa kupitia kompyuta kama vile kuangalia movie, kudownload movies hata za ukubwa wa 2GB, au hata kuangalia Youtube, n.k. Soma zaidi kuhusu teknolojia ya LTE katika makala yetu. 
 
Kuchaji simu bila kutumia waya:
Makampuni kadhaa kama vile ZTE, Google , AT & T, Starbucks na Nokia yamewekeza katika utafiti wa kuwa  na teknolojia itakayowezesha watumiaji wa simu kuchaji simu zao bila ya kuzichomeka ukutani . Kwa taarifa zilizopo kwenye mtandao wa Youtube, tayari Nokia wameshatoa simu zinazoweza kuchajiwa bila waya (wireless charging). Simu hizo za Nokia ni Nokia Lumia 920 na Nokia Lumia 820. Kampuni ya LG pia imetoa simu zake za LG Nexus 4 zinazotumia teknolojia ya wireless charging.
 
Website maalum za kuonekana kwenye simu:
Katika mabadiliko haya tunayoendana nayo ambapo watu wengi zaidi watatumia simu kuliko kompyuta, kuna haja basi ya kuwezesha websites ziwe na muonekano kama wa kwenye kompyuta za kawaida kwa watazamaji watakaotumia simu. Website hizo huitwa Mobile website. Kumbuka , kwa website kuwa Mobile website sio kwamba tuu eti inaweza kuonekana kwenye simu, hapana bali inakuwa imetengenezwa maalum kuwa na muonekano bora kwenye simu.
Mabadiliko yote haya yanamaanisha kuwa maisha yetu yanaenda kubadilika sana. Kuna ajira mpya na kuna watakaopoteza ajira au wateja. Mfano program mpya zinaendelea kubuniwa ili kurahisisha  matumizi ya simu ikiwa ni pamoja na kuwezesha simu kutype documents, kusave, kuprint, kama ambavyo watu wanafanya kwa kutumia desktop computer au laptops. Kwa wabunifu na watengenezaji wa website, wanatakiwa wajiboreshe katika kujua mabadiliko haya makubwa kwani tayari kuna muongozo wa jinsi ya kuprogram website ziendane na teknolojia za simu.
Wamiliki wa website na blogs wataanza kwa wingi kubadilika kuelekea kutumia teknolojia itakayofanya websites na blogs zao zionekane vema kupitia simu 

No comments:

Post a Comment