MAN UNITED WAPO KWENYE MAZUNGUMZO YA KUMRUDISHA CRISTIANO RONALDO OLD TRAFORD
Real Madrid wapo tayari kumuuza Cristiano Ronaldo kwenda Manchester United mwezi huu baada ya nahodha huyo wa Ureno kukataa kuanza mazungumzo ya mkataba mpya.
Gazeti la Daily Star limesema United na Real Madrid wametumia siku 12 zilizopita kuzungumza juu ya ada ya uhamisho ya paundi millioni 80 - na mabingwa wa Premier League wamezidi kupata uhakika wa kumrudisha kipenzi chao Old Trafford.
Raisi wa Real Florentino Perez mwanzoni alitaka kwamba uhakika kutoka kwa Ronaldo kama yupo tayari kusaini mkataba mpya - na alishangazwa kwamba mchezaji kuwa alikuwa tayari kurudi United.
Hilo lilipelekea Madrid kufungua mazungumzo rasmi na United, wakitambua kwamba wanaweza wakamuuza kwa fedha kidogo ikiwa winga huyo atabakia kwamwaka mmoja zaidi ndani ya Bernabeu kwa kuwa atakuwa amebakisha mkataba wa mwaka mmoja tu.
Lakini pia imeonekana wazi kwamba Madrid wanataka kumpata mbadala wa Ronaldo - Gareth Bale ambaye tayari wameshatoa ofa ya £85m kwa Spurs.
Mapema wiki hii aliyekuwa raisi wa Madrid - Ramon Calderon alikaririwa akisema kwamba Madrid wanajiandaa kumuuza Ronaldo na ndio maana wanafanya kila liwezekanalo kumsajili Gareth Bale kutoka Tottenham.
Ikumbukwe pia wakati akiwa bado kocha wa Man United Sir Alex Ferguson alikarriwa akisema kila kipo sawa kwa ajili ya usajili wa mchezaji mkubwa wakati wa dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa. Pia Wakati akihojiwa na BBC hivi karibuni aliyekuwa msaidizi wa Ferguson - Mike Phelan aliulizwa kama boss wake alikuwa akimzungumzia Ronaldo aliposema kuhusu usajili wa mchezaji mkubwa? Phelan alishindwa kukataa wala kukubali kuhusu suala hilo, akisema "no comment'.
No comments:
Post a Comment