Rais Jacob Zuma ametangaza muda mfupi uliopita kwamba mazishi ya Nelson
Mandela yatafanyika siku ya Jumapili, Desemba 15 kijijini kwake Qunu,
katika jimbo la Eastern Cape.
Rais Zuma pia ametangaza siku 10 za maombolezo kitaifa na bendera
zitapeperushwa nusu mlingoti katika muda wote huo. Na ameitangaza siku
ya Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya
maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi nzima.
Tayari msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria
umekamata dunia nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani, mstaafu
Bill Clinto na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ni baadhi tu ya
viongozi ambao wamethibitisha kushiriki.
Sala ya mazishi imepangwa kufanyika katika uwanja wa Taifa wa FNB Desemba 10, 2013 jijini Johanesburg.
Mwili wake utawekwa jengo la serikali liitwalo Union Buildings kuanzia
Desemba 11 hadi 13, kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya kupelekwa
kijijini Qunu kwa mazishi
Uwanja wa Taifa wa michezo wa Johannesburg ambako sala rasmi ya Kitaifa
ya mazishi itafanyika siku ya Jumapili ya Desemba 10, 2013
Jengo la Union Building ambapo mwili wake utawekwa kwa ajili ya kupewa heshima za mwisho kuanzia Desemba 11 hadi 13, 2013
Ulinzi mkali katika nyumba ya familia ya Madiba kijijini kwake Qunu
ambako atapumzishwa katika nyumba yake ya milele Desemba 15, 2013.
No comments:
Post a Comment